Wanajeshi wa
Ubelgiji wamemuua kwa kumpiga risasi mlipuaji wa bomu wa kujitoa
mhanga katika kituo kikuu cha reli mjini Brussels.
Polisi katika eneo la tukio
Waendesha mashtaka wanasema kuwa mshukiwa huyo amefariki.
Watu waliokuwa katika kituo Kikuu cha mabasi mjini Brussels na eneo la karibu la mnara ambalo hufurika watalii wote waliondolewa.
Wanajeshi wamekuwa wakilinda doria mjini Brussels tangu mwaka uliopita kulipotokea shambulio la kujitoa mhanga katika eneo la Uwanja wa ndege na kwenye mfumo wa usafiri wa chini ya ardhi.
CHANZO: BBC
SHARE









No comments:
Post a Comment