TRA

TRA

Thursday, June 8, 2017

TBS yakanusha kutangaza nafasi za ajira

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Mwandishi Wetu 


SIKU moja baada ya kusambaa taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetangaza nafasi za ajira, Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Profesa Egid Mubofu amejitokeza na kudai kuwa taarifa hizo ni za upotoshaji.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Profesa Mubofu alisema tangu kuanza kusambaa taarifa hizo potofu amepokea simu nyingi kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali kutaka kujua uhalali wake.


TBS 1
Prof. Egid Mubofu akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto Ofisa Uhusiano wa Shirika hilo, Roida Andusamile.

"Kumesambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa TBS imetangaza nafasi 200 za ajira, taarifa hizi si za kweli na naomba waliozipata wazipuuze.

“Taarifa hii imetusababishia usumbufu na hasa ukizingatia suala la kutangaza nafasi za ajira lina mamlaka zake kisheria na kuna utaratibu wa kutangaza ikiwemo kwenye magazeti, redio na televisheni au kupitia tovuti yetu, lakini kote huko taarifa hizi hazipo,” alisema.

Profesa Mubofu aliongeza:“ Nawaomba Watanzania walipuuze tangazo hili kwa sababu halijatolewa katika njia sahihi, kama kutakuwepo na taarifa za aina hiyo mtaziona kwenye vyombo vinavyotambulika na si kwenye mitandao ya kijamii.”

Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo aligusia nafasi ya shirika lake katika azma ya uchumi wa viwanda na kubainisha TBS ndiyo mdau mkubwa wa bidhaa za viwandani maana yake ongezeko la viwanda ni changamoto kwao kuimarisha huduma wanazotoa.

“Tanzania haiwezi kuingia katika uchumi wa viwanda bila TBS imara, hilo tumeliona na tumepanga mikakati ya kujiimarisha. Bidhaa zinazozalishwa lazima ziendane na viwango vya ubora vilivyowekwa na nchi na sisi ndio wasimamizi.

“Katika kuzingatia hilo tunao mpango wa kutengeneza maabara kubwa ya kisasa itakayopima ubora wa bidhaa zinazozalishwa nchini na zinazoingizwa kutoka nje ya nchi,” alisema Profesa Mubofu.

Aliweka wazi kuwa tayari zabuni ya kujenga maabara hiyo ya kisasa imetangazwa wakati wowote ujenzi utaanza. Kuhusu bidhaa zinazoingia nchini kupitia mipakani, Profesa Mubofu alisema:

"Tumejipanga kudhibiti bidhaa zisizofaa zinazoingizwa kupitia mipaka yetu ya nchi, tutaimarisha ofisi za kanda za TBS na kuzijengea uwezo ofisi za mipakani ili kuendana na kasi ya bidhaa zinazoingizwa bila kufuata utaratibu.”

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) lilianzishwa kwa Sheria ya Bunge- Sheria ya Viwango Na. 3 ya mwaka 1975, ilioyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 1 ya mwaka 1977. Ilipofutwa sheria hiyo ilichukuliwa na Sheria ya Viwango Na. 2 ya mwaka 2009.

Mbali ya kusimamia ubora wa bidhaa TBS pia wana jukumu la kutoa elimu kwa wazalishaji pamoja na wafanyakazi katika taasisi na viwanda kuhusiana na uzalishaji bidhaa bora, zalishaji salama na usimamizi wa ubora.


Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger