Kaimu Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Dkt. Doroth Gwajima akikata utepe kuzindua namba maalum itakayotumiwa na wananchi kuwasilina na Mamlaka hiyo ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa mkataba wa huduma kwa wateja. |
Kaimu Mkurugenzi wa Tiba toka
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Dkt. Doroth
Gwajima akisisitiza umuhimu wa Mamlaka ya Chakula na dawa (TFDA)
kuendelea kusimamia utoaji wa huduma zake katika viwango vya Kimataifa
wakati akizindua mkataba wa huduma kwa wateja wa Mamlaka hiyo leo
Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA ) Bw. Hiiti Sillo akizungumza wakati wa uzinduzi
wa mkataba wa huduma kwa wateja uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Tiba toka
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Dkt. Doroth
Gwajima (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi mkataba wa
huduma kwa wateja wa Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam kwa niaba
ya Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu.
Kaimu Mkurugenzi wa Tiba toka
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Dkt. Doroth
Gwajima (katikati) akionesha mkataba wa huduma kwa wateja wa TFDA mara
baada ya kuuzindua leo Jijini Dar es Salaam.kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA ) Bw. Hiiti Sillo na kushoto Mkurugenzi
wa Idara ya Uchambuzi na Usahuri wa kazi kutoka Ofisi ya Rais Utumishi na
Utawala Bora Bw. Mick Kiliba.
Kaimu Mkurugenzi wa Tiba toka
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Dkt. Doroth
Gwajima (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa TFDA mara
baada ya kuzindua mkataba wa huduma kwa wateja wa Mamlaka hiyo.
…………………………………………………………….
Frank Mvungi-Maelezo
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)
imezindua mkataba wa huduma kwa wateja ikiwa ni nyenzo mojawapo
inayowezesha kutolewa kwa huduma bora katika kiwango cha kimataifa na
kutekelezwa kwa vitendo juhudi za Serikali katika kuwahudumia wananchi
kwa weledi na uwajibikaji.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu
Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Doroth Gwajima wakati akizindua mkataba wa
huduma kwa wateja wa Mamlaka hiyo jana jijini Dar es Salaam kwa niaba ya
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu.
Akizungumza kuhusu mkataba huo
Dkt. Gwajima amesema kuwa ni jambo la faraja kuona kwamba uzinduzi wa
mkataba huu unafanyika katika kipindi cha maadhimisho ya wiki ya
utumishi wa umma mwaka 2017 ambayo msingi wake ni kutoa huduma bora
zinazoridhisha wateja kwa kuzingatia mkataba shirikishi wa huduma kwa
wateja.
“Nawapongeza TFDA kwani kwa
kutekeleza mkataba huu,watumishi wataweza kuepuka uzembe,upendeleo, na
rushwa mambo ambayo husababisha malalamiko kwa wananchi dhidi ya
watumishi na Serikali yao” Alisisitiza Gwajima.
Akifafanua amesema mkataba huo
utawezesha wateja kutambua haki zao, wajibu wao hali itakayosaidia TFDA
kuweka mfumo dhabiti wa upimaji wa viwango vya huduma (service
standards) kwa mujibu wa mkataba ili kubaini ufanisi wa mkataba huu na
kuchukua hatua stahiki za uboreshaji wa huduma pale inapobidi.
Aidha, alipongeza TFDA kwa kuweka
namba ya simu ambayo mteja anapiga bure wakati wa kazi, kuhusiana na
huduma zinazotolewa na TFDA ambayo ni 0800110084 na kuitumia
inavyostaili.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka hiyo Bw. Hiiti Sillo amesema utaratibu wa kuwa na mkataba wa
huduma kwa wateja umesaidia kuongeza tija ambapo kwa sasa huduma za
usajili wa maneno ya biashara za bidhaa zinazodhibitiwa na TFDA awali
zilitolewa ndani ya siku 45 mwaka 2006 na kufikia 2016 zinatolewa ndani
ya siku 10 tu.
Utoaji wa vibali vya kuingiza na
kusafirisha bidhaa nchini na nje ya nchi (Bidhaa zilizosajiliwa) mwaka
2006 zilitolewa ndani ya siku 5 na sasa ni siku moja tu, wakati usajili
wa dawa zinazozalishwa nchini awali ulikuwa unafanyika ndani ya siku 360
na sasa ni siku 120 tu.
Mkataba wa huduma kwa wateja
uliozinduliwa unaonesha ahadi za TFDA katika kuhudumia wateja wake na
pia wajibu wa wateja katika kuwezesha Mamlaka kuwahudumia kwa ufanisi
bila kuathiri ubora,Usalama na ufanisi wa
chakula,dawa,vipodozi,vifaa,tiba na vitendanishi.
Kwa mara ya kwanza,TFDA
ilitayarisha mkataba wa huduma kwa wateja kwa kushirikiana na wadau wake
mwaka 2006 na baadaye kurejewa mwaka 2012,marejeo ya mara kwa mara
yanatokana na msukumo wa mabadiliko ya kijamii,maboresho ya mifumo ya
utendaji,kuongezeka kwa rasilimali watu na ukuaji wa sayansi na
teknolojia katika utoaji huduma.
SHARE
No comments:
Post a Comment