Michuano ya kombe
la mabara inaendelea tena leo hii kwa michezo miwili ya kundi A
kuchezwa, wenyeji Urusi watashuka katika dimba la Otkrytiye Mjini
Moscow, kucheza na Ureno.
Na mchezo wa pili wawakilishi wa bara la Afrika katika michuano hiyo timu ya Cameroon watashuka katika dimba la Fisht Olympic kupepetana na New Zealand , mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi Bakary Gassama kutoka Gambia.
Urusi ndio vinara wa kundi A wakiwa na alama tatu baada ya kupata ushindi dhidi ya New Zealand, Ureno na Cameroon wao wana alama moja moja na New Zealand wanaburuza mkia wakiwa hawana alama hata moja.
CHANZO: BBC
SHARE









No comments:
Post a Comment