Ndege ya Urusi
ilipaa futi tano juu ya ndege ya ujasusi ya Marekani katika anga ya
bahari ya Baltic siku ya Jumatatu, kulingana na maafisa wa Marekani.
Lakini Urusi imepinga malalamishi hayo ya Urusi ikisema kuwa ndege hiyo ya Marekani iliichokoza ndege yake.
Ndege ya Marekani ya ujasusi aina ya US RC-135
- Urusi yaionya Marekani na kuitaka isiishambulie Syria
- Marekani yataka Urusi kuchunguzwa kwa uhalifu wa kivita
- Marekani yaapa kuichukulia hatua Urusi
Siku ya Jumanne, Jeshi la Marekani liliiangusha ndege isiokuwa na rubani inayomilikiwa na Iran nchini Syria na hivyobasi kuongeza wasiwasi kati ya Washington na Moscow ambayo ni mshirika mkuu wa utawala wa Syria.
Uchokozi huo wa siku ya Jumatatu ulifanyika kilomita 40 kutoka eneo la Urusi la Kalinigrad katika maji ya kimataifa.
Msemaji wa Pentagon Nahodha Jeff David aliambia maripota kwamba:Tulikuwa tukipaa katika maji ya kimataifa na hatukufanya uchokozi wowote.
CHANZO: BBC
SHARE









No comments:
Post a Comment