Kampuni ya
uchimbaji madini ya Acacia imekubali kuilipa serikali ya Tanzania
nyongeza ya mrabaa wa kati ya asilimia 4 mpaka 6 kama ilivyoainishwa
kwenye muswada wa sheria mpya ya madini nchini humo.
Serikali ya
Tanzania na kampuni ya Acacia ziliingia katika mgogoro mapema mwezi
tatu mwaka huu kutokana na kuzuiliwa kwa makontena 256 ya Mchanga wa
dhahabu (makinikia) kwenye Bandari ya Dar es Salaam baada ya kubainika
kuwa Acacia haitoi taarifa sahihi ya kiwango cha madini kilichopo katika
mchanga huo hivyo kulipa tozo zisizo sahihi kwa karibu miongo miwili
jambo ambalo linapingwa vikali na kampuni hiyo.
Rais Magufuli akihesabu makontena yenye mchanga wenye madini alipofanya ziara ya kushtukiza mwezi Machi
Licha ya kukubali kulipa ongezeko hilo Acacia imesema bado
inaendelea kutathimini athari zozote zinazoweza kujitokeza kutokana na
kuundwa kwa sheria hiyo mpya.
No comments:
Post a Comment