Mtu
mmoja aliyejulikana kwa jina la SULTAN YUSUPH, ambaye alikuwa utingo,
mkazi wa Kibaha Mkoani Pwani,amefariki dunia baada ya lori aina ya Howo
kupinduka katika Kijiji cha Gumbiro Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.Lori
hilo lililokuwa limebeba makaa ya mawe lilikuwa likitokea Kitai Wilaya
ya Mbinga Mkoani Ruvuma.
Kamanda wa Polisi Mkoani Ruvuma, GEMINI MUSHY
amesema kuwa dereva wa lori hilo amejulikana kwa jina la KAZI YUSUPH
na kwamba gari hilo ni mali ya kampuni ya Sun Shine ya Wilayani kibaha
mkoa wa pwani na kwamba chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa
gari hilo kuendesha gari kwa mwendo kasi.
Kamanda
MUSHY amesema hali ya dereva wa gari hilo inaendelea vizuri baada ya
kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kutokana na
majeraha aliyoyapata katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
Ametoa
wito kwa madereva kwamba jeshi hilo litaongeza kasi ya kuwapima kiwango
cha ulevi madereva wote ili kuondokana na ajali zinazo sababisha
kupoteza maisha ya Watanzania.
SHARE
No comments:
Post a Comment