Polisi nchini Australia imezuia njama ya kuidungua
ndege kwa kutumia milipuko ya kujitengenezea na ikawakamata watu wanne
baada ya kufanya misako majumbani katika viunga kadhaa vya mji wa
Sydney.
Waziri Mkuu Malcom Turnbull amesema usalama umeimarishwa katika
uwanja wa ndege wa Sydney tangu siku ya Alhamisi kwa sababu ya njama
hiyo. hatua hizo zilizoimarishwa za usalama pia zimewekwa kwenye viwanja
vyote vya safari za kimataifa na za ndani kote nchini Australia jana
usiku."nnaweza kuripoti kuwa jana usiku kumekuwa na operesheni kubwa ya kupambana na ugaidi ya kuzuia njama ya kigaidi ya kuiangusha ndege,". Turnbull amewaambia wanahabari.
"Kitisho cha ugaidi ni cha kweli. Operesheni hiyo ya kuzuia, juhudi za jana usiku zimekuwa za kufana lakini bado ipo kazi ya kufanywa".
Maafisa hawakueleza kama madai hayo ya njama yalihusisha safari ya kimataifa au ya ndani ya nchi, lakini gazeti la Sydney la Daily Telegraph limeripoti kuwa safari ya ndani ndiyo iliyolengwa.
Kamishna wa polisi nchini Australia Andrew Colvin ameitaja njama hiyo kuwa iliyoshawishiwa na itikadi kali za kidini, akisema wanaume wanne wamekamatwa katika misururu ya misako kote mjini Sydney siku ya Jumamosi.
Colvin amesema maafisa wa Australia walipokea "habari za uhakika kutoka kwa mashirika washirika" kuhusu madai lakini hakufafanua kama wanaume hao waliokamatwa walikuwa kwenye orodha hiyo. Aliongeza kuwa vitu kadhaa "vyenye umuhimu mkubwa kwa polisi" vilinaswa katika misako hiyo lakini polisi haikuwa na habari Zaidi kuhusu shambulizi maalum, wapi lingefanyika, tarehe wala muda. Amesema uchunguzi unatarajiwa kuchukua "mrefu zaidi "
Wanaume waliokamatwa, ambao umri wao haujatolewa na hawajashitakiwa na polisi, walikamatwa Jumamosi wakati polisi waliokuwa na silaha walivamia majumba katika vitongoji vinne vya Sydney
Jumla ya mashambulizi 12, kabla ya tangazo hili la karibuni kabisa, yamezuiwa katika miaka michache iliyopita, wakati watu 70 wameshitakiwa, amesema Waziri wa Sheria Michael Keenan.
Mashambulizi kadhaa ya kigaidi yametokea Australia katika miaka ya karibuni, ikiwa ni pamoja na uvamizi wa mkahawa mmoja mjini Sydney mwaka wa 2014 ambako mateja wawili waliuawa na mauaji ya polisi mmoja wa Sydney na mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 15.
SHARE
No comments:
Post a Comment