Klabu ya Besiktas
ya Uturuki imefanikiwa kumsajili bure beki kisiki wa timu ya taifa ya
Ureno, Képler Laveran Lima Ferreira, maarufu kama Pepe.
Mchezaji huyu aliachwa na klabu yake ya Real Madrid baada ya kumalizika kwa mkataba wake mwishoni mwa msimu uliopita.
Uhamisho huu wa mlinzi huyu unahitimisha miaka kumi ya kuitumikia Real Madrid ambapo alikua ni moja kati ya wachezaji muhimu wa kikosi cha kwanza wa timu hiyo.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment