Mwalimu wa zamani
aliyempiga Manny Pacquiao ili kushinda taji la uzani wa welterweight
ukanda wa WBO amepuuzilia mbali madai kwamba hakufaa kushinda taji hilo.
Mkufunzi wa Pacquiao na watu maarufu akiwemo Lennox Lewis na Kobe Bryant walikosoa matokeo hayo. Lakini bondia huyo wa Australia mwenye umri wa miaka 29 alisema kuwa alihitaji kushinda.
Kutakuwa na maneno kwamba nilikuwa na bahati ama chchote kile, aliwaambia maripota siku ya Jumatatu.
Kutakuwa na wale watakaosema kwamba sikuhitaji kushinda, lakini ninahisi kwamba nilishinda pigano hilo.
Wananchi wengi wa Queensland wanajua kwamba nilishinda pigano hilo pamoja na watu wote duniani.
Kocha wa Pacquiao nchini Australia Justine Fortune alitaja uamuzi wa refa na majaji kama usio wa haki kufuatia pigano hilo.
SHARE
No comments:
Post a Comment