Meneja wa
Manchester United, Jose Mourinho amedaiwa kutofurahishwa na taratibu za
usajili zinavyoendelea wa kipindi hiki cha majira ya kiangazi katika
klabu yake.
Man United haijafanikiwa kusajili wachezaji ambao kocha huyu anawataka katika kujenga kikosi kipya kwa ajili ya msimu ujao.
Kuna uwezekano kukawa na maendeleo mengine wiki hii lakini mpaka sasa ni mchezaji mmoja mpya aliyesajili ambaye ni beki Victor Lindelof toka Benfica ya Ureno.
Mourinho anahitaji mshambuliaji mmoja atakayeziba pengo la Zlatan Ibrahimovic, pamoja na kiungo mkabaji.
Man United wamekuwa wakimuwania mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata ambae uhamisho wake bado haujulikani hatima yake.
Lakini pia timu hiyo inawahitaji viungo Eric Dier wa Tottenham na Nemanja Matic kuja kujenga safu bora ya kiungo cha chini.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment