TRA

TRA

Saturday, July 15, 2017

China yaionya Botswana kuhusu Dalai Lama

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


 
China imeitahadharisha Botswana dhidi ya kumkubalia kiongozi wa kidini wa Tibet anayeishi uhamishoni Dalai Lama kuzuru taifa hilo mwezi ujao, shirika la habari la Reuters linasema.

Dalai Lama anatarajiwa kuhutubia kongamano kuhusu haki za kibinadamu katika mji mkuu wa taifa hilo la kusini mwa Afrika, Gaborone, mwezi Agosti na pia amepangiwa kukutana na Rais Ian Khama.

 Kiongozi wa kidini wa Tibet anayeishi uhamishoni Dalai Lama

Geng Shuang, msemaji wa idara ya mambo ya nje ya China anaripotiwa kuambia kikao cha wanahabari jijini Beijing mapema leo kwamba Dalai Lama alitumia cheo chake kujihusisha katika shughuli ambazo ni za kuihujumu China.
"Tunatumai kwamba taifa hilo linaweza kutambua hasa Dalai Lama ni nani, na kuheshimu wasiwasi wa China, na hivyo kuchukua uamuzi mwafaka kuhusu suala hili," taarifa yake ilisema.

Dalai Lama aliikimbia Tibet na kutorokea India karibu miaka 60 iliyopita baada ya kufeli kwa maasi aliyoyaongoza dhidi ya utawala wa China.

Kwa muda mrefu, amekuwa na uadui na China.
Serikali ya China humuita mtu hatari anayetetea kujitenga kwa Tibet, shirika la habari la Reuters linasema.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger