Na Kajunason Blog/Cathbert Kajuna.
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imevifungulia vituo vya mafuta vipatavyo
vitatu jijini Dar es Salaam baada ya kutimiza masharti ya kufunga
mashine za kielekitroniki zinazotoa risiti moja kwa moja kutoka kwenye
pampu ya mafuta (Automatic EFD).
Akizungumza
mara baada ya kufungua vituo hivyo, Kamishina wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), Charles Kichere amewashukuru wamiliki wa vituo hivyo kwa
kuonyesha ushirikiano kwa serikali kwa kutimiza masharti waliyopewa ya
kufunga mashine hizo na kusisitiza kuwa hakuna kituo kitakachofunguliwa
kama hakitatimiza masharti.
"Niwaombe
wamiliki wa vituo vilivyofungiwa kuwa kwa sasa hakuna
kitakachofunguliwa bila kutimiza mashart, timiza masharti tuje tukague
na tukufungulie uanze biashara yako," amesema Kamishna Kichere. Amesema
vituo vilivyofunguliwa leo ni GBP kilichopo eneo la Majumba Sita, Simba
Oil kilichopo eneo la Sitakishari, Ukonga na PETRO kilichopo eneo la
Kigamboni.
"Kitendo
cha kuunganisha mashine hizi na pampu za mafuta ni cha muda mfupi sana
na wala hakichukui muda mrefu, angalia huyu tulimfungia siku ya jumanne
tarehe 11 Julai na leo Ijumaa Julai 14 ameshafunga mashine na anaanza
kufanya biashara bila kugombana na serikali;" amesema Kamishna Kichere.
Mpaka
sasa vituo zaidi ya 40 vimefungiwa nchi nzima ikiwemo jijini Dar es
Salaam kwa kosa la kushindwa kufunga mashine za kielekitroniki zinazotoa
risiti moja kwa moja kutoka kwenye pampu ya mafuta (Automatic EFD). Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere
akikata utepe katika kituo cha mafuta cha Kigamboni jijini Dar es Salaam
baada ya kutimiza masharti ya kufunga mashine za kielekitroniki
zinazotoa risiti moja kwa moja kutoka kwenye pampu ya mafuta.
Mfanyakazi wa kituo cha mafuta cha Kigamboni akitoa risiti mara baada ya kuuza mafuta.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere akikagua risiti mara baada ya kuuza mafuta.
SHARE
No comments:
Post a Comment