Na Anil Ricco, Globu ya Jamii
Timu
ya Soka ya Everton inayoshiriki Ligi Kuu Soka nchini Uingereza (EPL)
inatarajiwa kuingia nchini Tanzania, July 12 kucheza Mchezo wake wa
Kirafiki na Klabu ya Soka ya Gor Mahia ya nchini Kenya, July 13 katika
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Everton inaingia nchini ikiwa na Gwiji wake wa Soka, Wayne Rooney aliyesajiliwa hivi karibuni.
Katika
mchezo huo baina ya Everton na Gor Mahia, Serikali kupitia kwa
Mkurugenzi wake wa Michezo, Yusuph Omary Singo amesema kuwa Mgeni rasmi
atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia
Suluhu Hassan.
Akithibitisha
ujio wa Kikosi hicho, Mkurugenzi wa SportPesa nchini Tanzania, Abbas
Talimba amesema maandalizi yote yamekamilika kwa Everton kutua nchini,
amesema Kikosi hicho kinakuja na Wanandinga wake wote.
Kwa
upande wa Upatikanaji wa Tiketi, Selcom kupitia Meneja Miradi na
Mshauri wa Mifumo, Galusi Lunyeta amesema watu watakaokuja kushuhudia
mchezo huo watahakikisha wote wanapata tiketi kupitia Mfumo huo wa
Selcom, kuanzia saa mbili asubuhi siku ya Mechi.
Pia
katika Suala la Ulinzi na Usalama, Inspekta wa Jeshi la Polisi, Hasheem
Abdallah amesema kuwa njia zitakazotumika kuingia Uwanjani siku ya
Mchezo huo katika Uwanja wa Taifa ni Mandela Road na Kilwa Road, watu
kufika Uwanjani na kutoka.
Mkurugenzi
wa Michezo, Yusuph Omary Singo akizungumza kwa niaba ya Serikali katika
kuupokea ugeni wa Timu ya Everton wanaokuja kucheza Mchezo wa Kirafiki
na Gor Mahia ya nchini Kenya, July 13 mwaka huu.
Mkurugenzi wa SportPesa nchini, Abbas Tarimba akifafanua jambo juu ya ujio wa Timu ya Everton ya Uingereza July 12 mwaka
Afisa
Usalama wa TFF na FIFA, Inspekta Hasheem Abdallah akifafanua kuhusu
Ulinzi katika Mchezo huo utakaopigwa July 13 katika Dimba la Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Meneja Miradi na Mshauri wa Mifumo - SELCOM, Galusi Lunyeta akifafanua juu ya upatikanaji wa Tiketi siku ya Mchezo huo July 13.
SHARE
No comments:
Post a Comment