Msanii
wa Bongo Fleva, Haitham amefafanua sababu ya Wema Sepetu kutoonekana
katika video ya ngoma yake mpya ‘Play Boy’ ambayo amemshirikisha mrembo
huyo.
Haitham
amesema kulikuwa na mipango ya kufanya video na Wema na script ilikuwa
tayari imeshaandikwa ila alipokosekana ilibidi wabadilishe.
“Na
script ambayo tumefanya sasa inayoonekana kwenye video wasichana watatu
ilibadilishwa fasta baada ya Wema kutokutokea kwenye video, so script
ya mwanzo ambayo Wema alipaswa kuwepo aliandika yeye director na baada
ya mabadiliko kutokea akabadilisha scrip,” ameiambia E-News ya EATV.
Kuhusu
athari zilizojitokeza baada ya Wema kutokuwepo kwenye video, amesema
“kwa upande wingine yameathiri kidogo sio sana kwa sababu kuna baadhi ya
mashabiki wa Wema walitamani kumuona kwenye video, kwa hiyo ameathiri
kidogo kwa wale mashabiki walikuwa wanatamani kumuona,” amesisitiza.
Play
Boy ni ngoma ya pili kwa Wema Sepetu kushirikishwa na msanii wa Bongo
Flava baada ya ile ya mwanzo ‘Shoga Yake Mama’ aliyopewa shavu na Snura,
lakini hizo zote hakuna hata moja Wema ametokea kwenye video.
SHARE
No comments:
Post a Comment