Na Zawadi Msalla-WHUSM.
Mkuu
wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka amewataka watendaji wa
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa mstari wa mbele
katika kutoa elimu kwa umma ya kuwa na utamaduni wa kutumia muda
kimkakati ili kufanya kazi kwa bidii na kufikia malengo.
Ayasema
hayo wakati wa mkutano na watendajin hao walipomtembelea ofisini kwake
wakati wa ziara ya kutembelea mikoa ya kusini mwa Tanzania kwa lengo la
kutembelea maeneo mbalimbali yanayojihusisha uhifadhi wa utamaduni
usioshikika kama vile mila na desturi za Watanzania.
“Utamaduni
wa kutumia muda kimkakati ni muhimu kwa Taifa na mtu binafsi kwa kuwa
inasaidia katika kuweka motisha ya kufanya kazi kwa bidii na hivyo
kufikia lengo lililokusudiwa” alisema Mhe. Ole Sendeka.
Aidha
aliongeza kwa kueleza kuwa falsafa ya mabadiliko ya utamaduni chanya ya
ufanyaji kazi ilianza tangu awamu ya kwanza ya uongozi wa Mwl. Nyerere
iliyokwenda kwa jina la Uhuru na Kazi na baadaye ikifuatiwa na kazi ni
kipimo cha Utu ambapo katika utawala wa awamu hii ya tano inaongozwa na
hapa kazi tu lengo ikiwa ni kufanya kazi kwa ajili ya kukuza uchumi
wetu.
Mhe.
Ole Sendeka anaeleza kuwa dhumuni za falsafa hizo ni kuhakikisha kuwa
kila mtu anatimiza wajibu wake wa kutumia muda kimkakati kwa kufanya
kazi ili kujenga Taifa bora lenye maendeleo.
“Endapo
elimu ya kutosha ya utamaduni wa kufanya kazi itatolewa ni imani kuwa
azma ya Mhe. Rais ya kuwatoa watanzania katika uchumi ulio nyuma na
tegemezi kwa kuwapeleka katika uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea
itawezekana” alisema Mhe. Ole Sendeka.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Prof. Elisante Ole Gabriel aliahidi kufanyia kazi mawazo hayo kwa
kuhakikisha jamii inapata elimu ya kutosha namna ya kuwa na utamaduni wa
kutumia muda kimakakati kwa kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo
yaliyokusudiwa.
Pia
alieleza kwamba ni kweli usiopingika ili Taifa liweze kufikia uchumi
wa viwanda ni budi kwa wananchi wake kujengea utamaduni wa kufanya kazi
kwa bidi ikiwemo kutumia muda kimkakati.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher
Ole Sendeka (kulia) alipofanya ziara ya kutembelea Mkoa huo.Picha na
Zawadi Msalla-WHUSM.
SHARE
No comments:
Post a Comment