Picha ya Pamoja wa pili kutoka kulia ni Naimbu kamanda wa umoja wa Vijana UVCCM Wilayani Tarime Mkoani Mara John Gimunta wa kwanza kulia ni Mwenyekiti UVCCM Wilaya ya Tarime Boniphace Mohere.
Picha ya pamoja katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorius Luoga ambaye pia ni Mjumbe wa NEC CCM baada ya kufungua kikao hicho. |
UMOJA wa vijana
wa Wilani Tarime mkoni Mara(UVCCM)
wameonywa kutotumia Rushwa katika Chaguzi ambazo zinatarajiwa kufanyika kwa lengo la kuwapata Viongozi wazuri wenye
maadili.
Kauli hiyo
imetolewa na John Gimunta ambaye ni Naibu kamanda wa UVCCM Wilayani Tarime katika kikao cha Baraza la Umoja wa UVCCM
kilichofanyika katika ukumbi wa jengo la CCCM wilaya kwa lengo la
kupitisha majina ya wagombea nafasi
mbalimbali kwenye kata ambao walichukua fomu na kurudisha.
Gimunta amesema
kuwa Wagombea wasitumie nafasi hiyo kushawishi wajumbe kwa kuwapa Rushwa ili
wawape kura na pia alionya wale ambao watashindwa katika kura za maoni kuacha
kuunda makundi na kuwa kufanya hivyo kunasababisha chama kugawanyika .
Hata hivyo
Gimunta amewataka vijana wa UVCCM kubuni
miradi mbalimbali ya mendeleo kwa lengo la kujipatia fedha ya kumudu maisha na
kuondokana na utegemezi
Mapema
Mkutano huo umlifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorius Luoga ambaye pia
ni Mjumbu wa NEC CCM ambapo amewataka vijana hao kufuata maadili ya Chama.
Aidha Luoga
amewataka vijana kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli katika uwekezaji wa Viwanda.
Mwenyekiti
wa UVCCM Wilaya Tarime,Boniphace Mohere amewataka wajumbe wa kikao hicho kutenda
haki kwa wagombea kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa .
SHARE
No comments:
Post a Comment