Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (The Foundation for Civil Society-
FCS), Bw. Francis Kiwanga akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa
katika Kongamano la siku moja la kuwahamasisha vijana kuchangamkia
fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Kongamano
hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza tarehe 19
Julai 2017.
Mkuu
wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Mary Onesmo Tesha ambaye alikuwa Mgeni
Rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella akisoma
hotuba ya ufunguzi kwenye kongmano la kuwhamasisha vijana kufanya
biashara za kuvuka mipaka ya nchi za EAC. Mhe. Tesha aliwasihi vijana
waondoe hofu na wajiunge katika vikundi ili waweza kufanya biashara kwa
urahisi. Aliahidi kutoa milioni moja kwa kikundi kilichoundwa hapohapo
kwa uratibu wa Mwkilishi wa Cloud Media, Bw. Samsonight Odera
Bi. Tesha akiendelea na hotuba yake.
Mchumi
kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw,
Justin Kisoka akiwaeleza vijana wa Mwanza waliofurika kwenye ukumbi wa
Rock City Mall sheria, kanuni na taratibu za kufuata kwa yeyote
anayetaka kuanza biashara ya kuvuka mipaka ya nchi za EAC.
Mtaalamu
wa Msauala ya EAC, Bw. Abel Maganya akitoa ufafanuzi wa masuala
mbalimbali kuhusu kufanya biashara ndani ya Jumuiya ya EAC ikiwemo namna
ya kupata cheti cha uasili na hati za kusafiria.
Mbinu
mbalimbali zilitumika kufikisha ujumbe wa umuhimu wa kufanya biashara
katika nchi za EAC. Hapa vijana wa Vipaji Foundation wakionesha kwa
kutumia igizo baaadhi ya bidhaa zinazoweza kuuzwa katika nchi za EAC.
Mjasiriamali
aliyefanikiwa ambaye pia ni maaruku wa kutoa mihadhara ya mbinu za
kufanya biashara, Bw. James Mwang'amba akiwasilisha mada kuhusu mbinu za
kuanza biashara na kuiendesha hadi ikakua kubwa.
Sehemu ya umati wa watu walioshiriki kongamano.
BABATI, MANYARA
Msafara
ulipokuwa unatokea Mwanza kwenda Arusha, ulisimama kwa muda Babati na
kuongea na Wanababati namna ya kufanya biashara katika nchi za EAC.
Mkazi wa Babati akiuliza swali ili apate ufafanuzi kabla ya kuanza kupeleka bidhaa zake nchini Kenya
Vijana wa Vipaji Foundation wakitoa somo kwa Wanababati kupitia sanaa.
Wanababati wakisikiliza kwa makini ujumbe wa namna ya kufanya biashara ya kuvuka mipaka.
SHARE
No comments:
Post a Comment