WATU wawili wamekufa katika matukio tofauti katika mkoa wa Rukwa,
akiwemo mkazi wa Kijiji cha Mafulala Manispaa ya Sumbawanga, Anna
Kashamsakula (35) aliyeuawa kikatili baada ya kuchinjwa na mumewe, baada
ya kumtuhumu kumhonga mwanamke mwingine Sh 30,000.
Mshtakiwa alipewa fedha hizo na mkewe ili akalipe kodi ya jengo,
waliyokuwa wakidaiwa na Mamlala ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Rukwa.
Akithibitisha, Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema
kuwa mauaji hayo yalitokea Julai 27, mwaka huu saa sita usiku katika
kijiji chaMafulala.
Akifafanua, alisema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi, ambapo
marehemu alimpatia mumewe Sh 30,000 ili akalipie kodi ya jengo, ambapo
hakulipa bali alienda kutumia na mwanamke mwingine.
Inadaiwa kuwa mume huyo alipewa kiasi hicho cha fedha na mkewe Julai 25,
mwaka huu, lakini hakurudi hadi siku iliyofuata, ambapo ugomvi wa
maneno uliibuka miongoni mwao hadi Julai 27, mwaka huu mume huyo
alipoamua kumuua mkewe na kutokomea kusikojulikana.
IMEANDIKWA NA PETY SIYAME, SUMBAWANGA
SHARE
No comments:
Post a Comment