MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeahirisha kesi inayowakabili mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Singh Sethi maarufu kama ‘Singasinga’ na mfanyabiashara James Rugemalira wanaokabiliwa na mashtaka 12, yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababisha serikali hasara.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 3 mwaka huu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya wakili wa serikali, kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.
SHARE
No comments:
Post a Comment