Izzo Business akitamba jukwaani katika tamasha hilo
Wasanii mbalimbali wakishiriki kumwaga moto wa burudani chini ya udhamini wa TBL
Mbunge
wa Ileje,Janeth Mbena (kulia) akibadilishana mawazo na Maofisa
Waandamizi kutoka TBL wakati wa tamasha hilo la kukata na shoka.
………………………………….
Mwanamuziki nguli
wa muziki wa kizazi kipya Izzo Business, mwishoni mwa wiki alimwaga
burudani kubwa kwa wakazi wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe katika bonanza la vijana na ujasiriamali ambalo lilifanyika katika kituo cha mabasi ya Itumba likiwa limeandaliwa na mbunge wa jimbo hilo, Janeth Mbena, na kufadhiliwa na kampuni ya TBL.
Izzo Business aliweza kuwapagaisha washabiki wa muziki wa bongo Fleva
kutoka mwanzo wa onyesho hadi mwisho ambapo pia kulikuwepo burudani za
kila aina kutoka wasanii mbalimbali chipukizi mkoani Mbeya na kabla ya onyesho vijana walipatiwa mafunzo ya mbinu za ujasiriamali.
Mbunge wa jimbo hilo Janeth Mbena ambaye alikuwa
mgeni rasmi alisema kuwa lengo la tamasha hilo ni kuwaleta vijana
pamoja kwa kuwapatia maarifa na mbinu za maisha ikiwemo kuwaletea burudani na alitoa shukrani kwa TBL na wadau wengine kwa kulifanikisha.
Meneja
Mawasiliano wa TBL Group,Zena Tenga ,akiongea udhamini huo alisema kuwa
kampuni ya TBL Group kupitia moja ya sera yake ya ‘Kujenga Dunia
Maridhawa’ imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inatoa kipaumbele
kudhamini michezo na burudani za muziki lengo likiwa ni kuleta burudani
kwa jamii na kukuza vipaji vya wanamichezo na wasanii.
Tenga alisema TBL
imevutiwa na mkakati wa kuwapatia vijana elimu ya ujasiriamali ambao
umeanza kutekelezwa wilayani Ileje.”Vijana ni kundi muhimu sana katika
ukuzaji uchumi wa nchi hivyo wanahitaji kupata mbinu za kukabiliana na
changamoto mbaimbali za maisha”.
Alimalizia kwa
kusema kampuni ya TBL nayo inatekeleza mpango wa kutoa elimu kwa
wajasiriamali sambamba na kutoa elimu ya unywaji wa kistaarabu lengo
likiwa ni kujenga jamii ya watu makini ambao wanatumia vinywaji kwa ajili ya afya na burudani na sio kwa ajili ya kuwa walevi na kuleta usumbufu kwenye jamii.
SHARE
No comments:
Post a Comment