Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa
Kodi, wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo,
akizunhuzma na waandishi wa habari makao makuu ya Mamlaka hiyo jijini
Dar es Salaam leo Julai 11, 2017. Pamoja na mambo mengine, Bw. Kayombo
alisema Mamlaka hiyo imekusanya kiasi cha Shilingi Trilioni 14.4 kwa
mwaka wa fedha wa 2016/2017.
NA K-VIS
BLOG/Khalfan Said
MAMLAKA ya
Mapato Tanzania, (TRA), imekusanya kiasi cha shilingi Trilioni 14.4 kwa mwaka
wa fedha wa 2016/2017, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi, Bw.
Richard Kayombo, amewaambia waandishi wa habari leo Julai 11, 2017.
Bw.
Kayombo alisema makusanyo hayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 7.67
ikilinganishwa na makusanyo ya mwaka 2015/2016 ambayo yalikuwa ni kiasi cha
shilingi Trilioni 13.3.
Aidha kwa
niaba ya Mamlaka, Kayombo amefurahishwa na muitikio wa wananchi katika
kulipa kodi ya majengo na kwa wale wanaoendeleakujitokeza katika ofisi za TRA
kote nchini kulipa kodi hiyo ambayo mwisho wa kulipa kodi hiyo kwa mwaka wa
fedha unaoishia Julai ni tarehe 15/07/2017.
. “Mwaka
wa fedha umeshaanza, wananchi wanaweza kuanza kulipa kodi hiyo sasa, na hii itasaidia
kuondoa usumbufu, maana viwango vya kodi ya majengo vinajulikana.” Alisema Bw.
Kayombo.
Kuhusu
matumizi ya risiti za kielektroniki, Kayombo ametoa wito kwa
wafanyabiashara kote nchini kutoa risiti za EFD pindi wanapouza bidhaa au kutoa
huduma na wananchi wote kuhakikisha wanadai risiti za EFD pindi wanaponunu
bidhaa au huduma na kwa kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa
kwa yeyote atakayekutwa na kosa la kutokutoa risiti.
“ Hivi
sasa kuna zoezi la uhamasishaji na ukaguzi linaloendelea nchi nzima katika
sehemu zote za biashara kukagua wafanyabiashara wasiotumia Mashine za Risiti za
Kielektroniki za EFDs pamoja na wananchi wote wasiodai risiti baada ya kununua
bidhaa au huduma.” Afafanua. Na kuongeza, Napenda kuwakumbusha wananchi wote
kuhakiki risiti zao ili kuona usahihi wake ikiwa ni pamoja na tarehe, na mkiasi
walicholipa kabla ya kuondoka na risiti hiyo.” Alisisitiza.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Kayombo (kulia)
Waandishi wakiwa kazini.
Kayombo akiendelea kufafanua masuala mbalimbali yahusuyo kodi.
Mwandishi wa habari mwandamizi wa Channel 10, Kibwana Dachi, akirekodi taarifa ya Kayombo.
Bw. Dachi, akiuliza swali.
Ofisa Habari Mwandamizi wa TRA,
Rachael Mkundai, (katikati), Ofisa Habari, Mariam Mwayela, (kulia),
na Ofisa Msaidizi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Chama Siriwa wakijadiliana jambo.
Waandishi wa habari, wakiwa makini kazini.
SHARE
No comments:
Post a Comment