Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki
(kushoto) akipokea vitabu vya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998
kutoka Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mpingo Conservation
Initiatives, Makala Jasper ambalo limesaidia kuchapisha nakala 1304 za
sera hiyo kwa ajili ya kusaidia zoezi linaloendelea la kuboresha Rasimu
ya Sera Mpya ya Misitu ya Mwaka 2016 katika warsha iliyoandaliwa na
Wizara hiyo mjini Dodoma leo. Kulia anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Idara
ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezeckiel Mwakalukwa. (Picha na Hamza
Temba-Wizara ya Maliasili na Utalii)
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili
na Utalii, Alen Richard akizungumza na baadhi ya wadau wa Misitu wakati
wa warsha iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa ajili ya kuboresha
Rasimu ya Sera Mpya ya Misitu ya mwaka 2016 lililoandaliwa na Wizara
hiyo mjini Dodoma leo. (Picha na Hamza Temba-Wizara ya Maliasili na
Utalii)
SHARE
No comments:
Post a Comment