TRA

TRA

Monday, July 17, 2017

HOFU YATANDA ARSENAL KUHUSU THOMAS LEMAR

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
 
Arsenal wanaamini kwamba huenda wakapoteza nafasi ya kumnunua mchezaji ambaye wamekuwa wakimtafuta sana, Thomas Lemar wa klabu ya Monaco.

Gunners bado wanatia juhudi kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa wa umri wa miaka 21 lakini sasa kumeibuka wasiwasi kwamba mabingwa hao wa Ufaransa huenda wasitake kumuuza.

Hii ni baada ya Monaco kuwauzia Chelsea kiungo Tiemoue Bakayoko.


 Thomas Lemar

Mchezaji wao mwingine Benjamin Mendy anatarajiwa pia kuwaaga, jambo ambalo linaifanya vigumu kwao kumuuza Lemar.
Hayo yakijiri, Arsenal wamesalia kufanya kila wawezalo kumzuia Alexis Sanchez kuondoka.

Mchezaji huyo wa Chile anaingia katika mwaka wake wa mwisho katika mkataba wake wa sasa katika kalbu hiyo na anadaiwa kutaka kuondoka, lakini Gunners wanataka kumkwamilia.
Alikuwa mfungaji bora wao msimu uliopita.
Monaco walimuuza Bakayoko kwa Chelsea kwa £40m, naye beki wa kushoto Mendy anahusishwa na kuhamia Manchester City.
Kuna pia tetesi kwamba mshambuliaji wao Kylian Mbappe, 18, ambaye pia anatafutwa na Arsenal na Real Madrid anaweza kuondoka.
Arsenal kipindi hiki wamemnunua mshambuliaji Alexandre Lacazette kutoka Lyon kwa £46.5m ambayo ni rekodi kwao.
Walimchukua pia beki wa kushoto Sead Kolasinac kutoka Schalke bila kulipa ada yoyote baada yake kuwa amemaliza kutumikia mkataba wake.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger