TRA

TRA

Sunday, July 16, 2017

Jeshi la Australia lapewa nguvu mpya kukabiliana na ugaidi

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Jeshi la Australia limepewa nguvu mpya kukabiliana na ugaidi ndani ya nchi.

Serikali ilipendekeza mabadiliko ya sheria za ulinzi wa nchi kama njia mpya ya kukabiliana na ugaidi.

 Waziri mkuu wa Australia Malcolm Turnbull
Hatua hio mpya inamaanisha kuwa jeshi la Australia litaitwa hivi karibu kusaidia polisi kukabiliana na vitisho.

Hii imetokana na shatuma kuhusu jinsi polisi waliitikia kisa cha ugaidi cha mwaka 2014 mjini Sydney. 

Sheria ya sasa inazuia polisi kuwaita jeshi hadi pale watakapohisi kuwa wamelemewa. Chini ya hatua mpya, jeshi pia litatoa mafunzo maalum kwa Polisi.
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Waziri mkuu Malcolm Turnbull alisema kuwa anataka kuwepo ushirikiano kati ya polisi na jeshi.

Mateka wawili na mshambuliaji waliuawa wakati wa kisa cha mjini Sydney mapema mwaka huu.

CHANZO: BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger