Kesi inayowakabili
viongozi wakuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Rais Jamal Malinzi
na Katibu wake, Selestine Mwesigwa imeahirishwa tena hadi Agosti 11 ili
kupisha upepelezi zaidi.
Viongozi hao wakiwa pamoja na Mkurugenzi wa Fedha wa TFF,
Isinde Isawafo Mwanga walifikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu
mjini Dar es Salaam, kwa mara ya nne na kusomewa mashitaka yao 28,
Hakimu mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbroad Mashauri, alisema
anaiahirisha kesi hiyo tena kwa sababu upelelezi haujakamilika na
washtakiwa wanarudi rumande hadi Agosti 11 kesi hiyo itakapotajwa tena.
Malinzi, pamoja na Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa na
Mhasibu, Nsiande Isawafo Mwanga walipelekwa rumande Juni 29 baada ya
kusomewa mashitaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti
ya TFF iliyopo katika banki ya Stanbic, Dar es Salaam.
Katika mashitaka hayo, 25 yanakwenda moja kwa moja kwa Rais wa
shirikisho hilo, Malinzi akidaiwa kughushi michakato mbalimbali ya
kifedha, huku matatu yakiwahusu wote na Katibu wake na Mhasibu wake
Nsiande Isawafo Mwanga.
Malinzi aliingia madarakani TFF Oktoba mwaka 2013 baada ya
kupata kura 72 kati ya 126 zilizopigwa akimshinda aliyekuwa mpinzani
wake wa karibu, Athumani Nyamlani.
Lakini baada ya kesi hii kuanza kuunguurma na kuwekwa rumande,
Kamati ya Utendaji ya TFF ilikutana na kumteua Makamu wake, Wallace
Karia kukaimu Urais wa shirikisho hilo.
Lakini kwa mwenendo wa kesi, Malinzi ndiyo kama amekwishaaga
TFF, kwani uchaguzi unatarajiwa kufanyika Agosti 12 mjini Dodoma naye
hajashiriki usaili wa wagombea, hivyo haruhusiwi tena kugombea.
Wakati huo huo: Kesi zinazowakabili viongozi wa klabu ya Simba,
Rais Evans Eilieza Aveva na Makamu wake, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ nayo
imeahirishwa hadi Agosti 7, mwaka huu kwa sababu pia upelelezi
haujakamilika.
Aveva na Kaburu wanakabiliwa na mashitaka matano yakiwemo ya
utakatishaji fedha, ambayo hayana dhamana na wote wapo rumande gereza la
Keko tangu Juni 29.
Wawili hao leo waliletwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar
es Salaam kwa mara ya nne na kusomewa tena mashitaka hayo kabla ya
Hakimu Victoria Nongwa kuiahirisha tena kesi hiyo hadi Agosti 7, mwaka
huu.
Miongoni mwa mashitaka yanayowakabili ni pamoja na kughushi nyaraka zinazodaiwa kuwa klabu ya Simba inawalipa madeni watuhumiwa hao kiasi cha dola za Kimarekani 300,000 (Zaidi ya shilingi milioni 700 za kitanzania). Makosa mengine ni Aveva kutoa nyaraka za uongo kwa Benki ya CRDB Tawi la Azikiwe Dar es Salaam Machi 10, 2016, la tatu ni kutakatisha fedha kinyume cha sheria, ambapo inadaiwa rais huyo na Kaburu walikula njama za kufanya uhalifu huo. Shtaka la nne ni Kaburu kutakatisha fedha dola 300,000 na kuziweka katika Benki ya Barclays Tawi la Mikocheni mjini Dar es Salaam, na la tano ni kutakatisha fedha likimhusu tena, Makamu wa Rais, Kaburu anayedaiwa kumsadia Aveva kutakatisha fedha katika benki ya Barclays baada ya kughushi nyaraka.

SHARE
No comments:
Post a Comment