Katika kuhakikisha Wananchi wanalindwa na kuhakikisha wanaishi katika mazingira salama Serikali imezindua kifaa hicho ambacho kina uwezo wa kugundua kemikali zenye sumu kwenye maji taka ambayo hutiririshwa kutoka viwandani na kusambaa kwenye mazingira ya wananchi.
“Kuna haja ya kufanya uchunguzi wa kupima ubora wa maji katika mito hasa hii ya Dar es Salaam kutokana na uchafunzi mkubwa wa mazingira unaoendelea. Tayari nimeagiza mito mitano ipimwe; Mto Msimbazi, Mto Mlalakuwa, Mto Kibangu, Mto Ng’ombe na Mto Kijitonyama. Mito hii ipimwe tuone ubora wake wa maji ukoje.
“Viwanda vingi ambavyo havina mfumo wa kutibu maji taka…maji taka yanayozalishwa viwandani yanatiririshwa moja kwa moja kwenda kwenye mazingira na kuja kwenye mto.” – Luhaga Mpina.
SHARE
No comments:
Post a Comment