TRA

TRA

Tuesday, July 11, 2017

KILA KONA MJADALA SASA NI WAYNE ROONEY

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
 
MAKAMU wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan atapata fursa ya kumsabahi mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney kabla ya timu yake mpya, Everton kumenyana na Gor Mahia Alhamisi mjini Dar es Salaam. Refa maarufu nchini, Israel Mujuni Nkongo ndiye atachezesha mchezo huo wa kirafiki kati ya Everton ya England na Gor Mahia ya Kenya Uwanja wa Taifa, Jijini. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Utawala na Uendeshaji wa SportPesa Tanzania, Tarimba Gulam Abbas amesema kwamba maandalizi yote ya mchezo huo yamekamilika na Everton wataingia nchini kesho asubuhi.
Everton wanatarajiwa kuja na Wayne Rooney na watavaa jezi hizi za ugenini keshokutwa
“Everton wanaingia kesho majira ya asubuhi na Alhamisi watacheza mchezo wa kirafiki na timu kutoka nchini Kenya, Gor Mahia,”amesema Mwenyekiti huyo wa zamani wa klabu ya Yanga. Aidha, Mkurugenzi huyo Mkuu wa zamani wa Bodi ya Michezio ya Kubahatsha nchini amesema kwamba mgeni rasmi katika mchezo huo wa kihistoria atakuwa ni Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan. Gor Mahia ilipata nafasi ya kucheza na Everton baada ya kuibuka bingwa wa michuano ya SportPesa Super Cup, ikiwafunga mahasimu, AFC Leopatrds 3-0

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger