Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb.) akiongea na
baadhi ya wananchi wa mtaa wa Mivinjeni Buguruni Sukita alipowatembelea kufuatia kero ya utiririshwaji wa maji yanayosadikiwa
kuwa na kemikali kutoka katika baadhi ya viwanda maji yanayotumiwa na
wakazi wa maeneo hayo kwa kumwagilia bustani za mboga mbonga. Kutoka
kulia kwake ni Naibu Meya wa wa Manispaa ya Ilala, Omary
Kumbilamoto, Afisa Mazingira Ilala Bw. Adon Mapunda na Diwani wa kata ya
Buguruni, Adam Fugane.
Naibu Waziri Mpina Akiongea na Wanahabari katika Bonde Buguruni Sukita jijini Dar es Salaam alipofanya Ziara leo.
Bwana Jafari Chimgege mratibu wa
Mazingira kutoka Baraza la Taifa la usimamizi na Hifadhi ya mazingira
NEMC kanda ya mashariki akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Mpina kuhusu
Kiwanda cha ANBANGS kinachomilikiwa na raia wa China kivyokaidi kutoa
faini ya shilingi milioni 25, iliyotozwa mwaka jana mwezi November
kutokana na uchafuzi wa mazingira.
Pichani ni kijana ambaye jina
lake halikupatikana akimwagilia maji yanayosadikiwa kuwa na kemikali
mbogamboga aina ya majani ya Maboga zinazochipua katika eneo la mtaa wa
mivinjeni buguruni sukila, leo. (Habari na Picha na Evelyn Mkokoi wa
OMR)
…………………………………………………………………….
Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira NEMC limepewa siku saba kukagua na kujiridhisha
na uzalishaji, management na utekelezaji wa sheria ya mazingira ya mwaka
2004 na kanuni zake kwa Kiwanda cha ANBANGS kinachotengeneza mifuko
aina ya viroba vinavyotumika kama vifungashio vya saruji, sukari na aina
nyingine ya nafaka, na kukifunga kwa kile kinachodaiwa kukaidi maagizo
ya serikali ya awamu ya tano ya kutokulipa faini kwa uchafuzi wa
mazingira.
Naibu Waziri Ofisi ya Makmu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alitoa agizo hilo Leo
alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Buguruni baada ya kupata
malalamiko yaliyoibuliwa na wakazi wa mtaa wa sukita mivinjeni kupitia
kituo cha ITV ambapo Naibu waziri Mpina alitembelea eneo hilo na
kujionena namna ambavyo kiwanda hicho kinavyoendelea kutiririsha maji
machafu.
Akiwasilisha taarifa ya ukaguzi
wa kiwanda hicho Bw. Jafari Chimgege ambae ni Mratibu wa mazingira
kutoka NEMC kanda ya Mashariki alimueleza Naibu waziri Mpina, kuwa “Kama
unakumbuka Mhe. Waziri Tulikuja hapa mwaka jana Novemver na tukafanya
ziara na ukaguzi hapa na kila tukija hapa hawa wachina wanashindwa
kuonyesha ushirikiano na kusema kuwa wao hawajui lugha ya Kiswahili,
tuliona makosa mengi na tuliwatoza faini ya shilingi milioni 25, na
ilitakiwa walipe ndani ya wiki mbili, lakini Mhe. Hiyo Faini haikulipwa.
Na bado wanaendelea na uchafuzi wa mazingira pamoja na kukaidi agizo za
serikali.” Alisisistiza Chimgege.
Pamoja na maelezo hayo ya Bw. Chimgege Naibu Waziri alielekeza Baraza hilo kupitia documents
zote muhimu zinazohusu, kiwanda hicho ambacho awali hakikuwa na cheti
ya tathmini ya athari ya mazingira wala vibali ya aina yoyote ya
kutirirsha maji yaliyotibiwa na kuuganishwa na mfumo wa mji taka wa
DAWASCO hali ambayo ilimpelekea Mpina pamoja na hilo kuagiza wamiliki wa
kiwanda hicho kufikishwa mahakamani
Katika Ziara zake za ukaguzi wa
Mazingira na viwanda jijini Da es Salaam, Mpina amehadi kuingia hatua ya
kushirikiana na mamlaka husika kuchukua sampuli za maji yanayopita
katika bonde la mto msimbazi katika eneo la viwanda vya karibu na mtaa
wa sukita mivinjeni ili kuyafanyia vipimo na kijirisha kama yana madhara
kwa viumbe hai na mazingira hususani mboga mboga zinazomwagiliwa maji
katika maeneo.
SHARE
No comments:
Post a Comment