Mchezaji wa Ajax, Abdelhak Nouri.
SIMANZI
imerudi tena kwa wachezaji, viongozi na mashabiki wa Ajax, baada ya
kusikia kuwa mpendwa wao, Abdelhak Nouri, yupo katika hali mbaya na
hakuna uwezekano wa kupona.
Kinachowaumiza
wengi ni kwamba kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20, akiwa na umri
mdogo mno, amepata masaibu makubwa yanayomfanya asiwe tena na nafasi ya
kufikia ndoto zake.
Familia yake imethibitisha juzi kuwa wameambiwa na madaktari kwamba dogo huyo hawezi kupona.
Dogo huyo
alianguka ghafla uwanjani baada ya kukumbwa na tatizo la moyo akiwa
katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na msimu mpya, dhidi ya Werder
Bremen wikiendi moja iliyopita.
…Akiwa katika pozi.
Nouri
alikimbizwa haraka hospitali akiwa hajitambui na k u w e k e w a
mashine za kumsaidia kupumua.Lakini baada ya kuamka, sasa dogo huyo kwa
huzuni nyingi, amepata tatizo kubwa na la kudumu la ubongo kutokana na
upungufu wa oksijeni.
Kwa
majonzi makubwa, kaka wa Nouri ameweka wazi kuwa kiungo huyo hataweza
tena kutembea, kuzungumza na hataweza pia kuitambua familia yake, huku
nafasi ya kupona ikiwa sawa na sifuri.
Hakika
maisha hubadilika ghafla sana kuliko unavyofikiri. Wiki mbili
zilizopita hakuna ambaye alitarajia dogo huyu leo hii atakuwa katika
hali hii ya ufu.
Abderrahim,
ambaye ni kaka wa Nouri, anasema: “Hataweza kutembea, hataweza
kuzungumza, hatambui sisi ni akina nani, yaani hatujui kabisa. Hahisi
chochote, hasikii chochote.
“Jana (juzi) asubuhi, madaktari walimfanyia vipimo vingine. Eneo kubwa la ubongo limeathirika na halifanyi kazi.
“Kwa
mujibu wa madaktari, hatafanya tena hayo milele, hatapona. Lakini
namuamini Allah. Ikiwa hivyo mwisho wa siku nitakubali. Ni kijana mzuri.
Kila mtu, dunia nzima, anaongea vitu vizuri kuhusu yeye.
“Dini
yetu inatufundisha kukubaliana na kinachotokea na tunaomba kwa ajili ya
uponyaji wake. Mpaka sasa tunashikilia ukweli huo. Hata hivyo,
tunaamini kuwa maisha haya ni mafupi na kwamba maisha ya milele
yatafuata, lakini kila mmoja alitarajia kumuona akifunga mabao
kwanza.”
Dada wa Nouri, Ghizlan, anaongeza: “Tunatumaini kwamba siku moja mambo yote yatakuwa mazuri kwa kijana wetu mzuri Nouri.”
Tangu
apatwe na masaibu hayo, Nouri ambaye aliibuliwa katika akademi ya Ajax
mwaka juzi, amekuwa akipokea sapoti mbalimbali kutoka kwa familia ya
soka huku majirani wakiwa wamepiga kabisa kambi nje ya nyumba yake
wakiomboleza.
Hata
mahasimu wakubwa wa Ajax, PSV Eindhoven, wameonekana kuhusika kutoa
faraja katika kipindi hiki kigumu huku mastaa wakubwa wa Uholanzi,
Robin van Persie na Georginio Wijnaldum wakiwa tayari wameshatoa sala
zao.
SHARE
No comments:
Post a Comment