Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amefikishwa katika Mahakama ya Kisutu leo asubuhi ili kusomewa mashtaka ya kesi yake inayomkabili.
Mdee,
alikamatwa na Polisi siku sita zilizopita kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, Ali Hapi kwa madai ya kumkashifu Rais John Magufuli.
Hapi aliagiza Mdee akamatwe na kuwekwa ndani kwa saa 48 kwa makosa hayo pamoja na ya uchochezi.
UPDATES
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemsomea shtaka la kutoa lugha ya matusi Mbunge Halima Mdee, ambaye amekana shtaka hilo na kuachiwa kwa dhamana ya Tsh. Milioni 10.
Akisoma
shtaka hilo, Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi
Victoria Nongwa alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo
Baada
ya kukana shtaka hilo Hakimu alisema mshtakiwa huyo ambaye wakili wake
ni Peter Kibatala ana haki ya kupewa dhamana, ndipo akadhaminiwa na
madiwani wawili wa Chadema (majina hayajapatikana) pamoja na yeye
mwenyewe kwa bondi ya Tsh. Milioni 10 huku kesi hiyo ikiahirishwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment