Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu
za Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigwabo (kushoto),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam
leokuhusu mfumuko wa bei wa Taifa kwa Mwezi Juni. Kulia ni Meneja wa
Takwimu za Bei na Ajira, Ruth Minja.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwezi Juni
umepungua hadi kufikia asilimia 5.4 ikilinganishwa na asilimia 6.1
ilivyokuwa mwezi Mei 2017.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa
Sensa na wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo
mchana kuhusu mfumuko huo wa bei.
Kwasigabo alisema kasi hali hiyo
inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka
ulioishia mwezi Mei 2017 imepungua zaidi ikilinganishwa na kasi
iliyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2017.
"Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 109.10 mwezi Juni,2017 kutoka 103.47 mwezi Juni 2016" alisema Kwesigabo.
Alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za
vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Juni 2017 umepungua hadi hadi
asilimia 9.6 kutoka asilimia 11.6 ilivyokuwa mwezi Mei,2017
Alisema mfumuko wa bei kwa kipimo cha
mwaka kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Juni 2017
umepungua hadi kufikia asilimia 9.8 kutoka asilimia 11.8 mwezi Mei 2017.
Aliongeza kuwa badiliko la fahirisi za
bei kwa bidhaa zisizo za vyakula umeongezeka hadi asilimia 3.11 mwezi
Juni 2017 kutoka asilimia 3.1 mwezi Juni, 2017 kutoka asilimia 3.0 mwezi
Mei 2017.
SHARE
No comments:
Post a Comment