Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Ubungo,John Lipesi Kayombo akizungumza na wananchi
pamoja na wafanyabiashara katika soko la Ndizi-Mabibo wakati wa ziara ya
kikazi katika eneo hilo.
Wananchi pamoja na wafanyabiashara katika soko la Ndizi-Mabibo wakifatilia kwa makini mkutano
Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Ubungo, John Lipesi Kayombo akitafakari kwa makini
changamoto mbalimbali za wananchi pamoja na wafanyabiashara katika soko
la Ndizi-Mabibo wakati wa ziara ya kikazi katika eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Kisare Makori (Kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya
Ubungo, John Lipesi Kayombo wakati wa ziara ya kikazi katika soko la
Ndizi-Mabibo
Wakuu wa Idara na Vitengo
Manispaa ya Ubungo wakifatilia mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe
Kisare Makori uliofanyika katika Soko la Ndizi-Mabibo Jijini Dra es
salaam
Wananchi
pamoja na wafanyabiashara katika soko la Ndizi-Mabibo wakifurahi mara
baada ya kuambiwa wataendelea na shughuli zao katika soko hilo.
…………………………………………………………………..
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Ubungo amebaini ubadhirifu wa kiasi kikubwa cha pesa
zinazofikia shilingi milioni tisini kila mwezi, unaofanywa na kikundi
kinachojiita Majimoto kinachodai kupewa jukumu la kukusanya mapato
katika soko la matunda la Mabibo kwa niaba ya mmiliki wa eneo hilo
ambaye ni Kiwanda cha Nguo cha Urafiki.
Mkurugenzi Kayombo amesema kuwa
ubadhirifu huo umebainika baada ya Halmashauri ya Manispaa kuchukua
jukumu la kusimamia kwa muda ukusanyaji mapato katika soko hilo ambapo
makusanyo yamepanda kutoka shilingi milioni saba zilizokuwa zinakusanywa
hapo awali hadi zaidi ya shilingi milioni mia moja.
Kayombo amesema hayo wakati wa
ziara ya ghafla iliyofanyika sokoni hapo na kuongozwa na Mkuu wa Wilaya
ya Ubungo Mhe Kisare Makori kwa ushirikiano wa pamoja na Wakuu wa Idara
na Vitengo sambamba na watendaji wote katika Manispaa hiyo,
Ziara hiyo imejili mara baada ya
uongozi wa kiwanda cha Urafiki kutaka kuwaondoa kwa nguvu
wafanyabiashara na kulifunga eneo hilo kwa kujenga uzio utakaozuia
ufanyaji wa biashara.
Mkurugenzi amejibu hapo hapo
agizo la Mkuu wa Wilaya Mhe Makori lilomtaka kusitisha mara moja zoezi
la kuwaondoa wafanyabiashara hao kwa kuwaagiza Afisa Afya na Mazingira
wa Manispaa ya Ubungo kufuatilia malalamiko yaliyotolewa na wananchi
katika mkutano huo kuhusu kiwanda cha nguo cha Urafiki ambacho
kinalalamikiwa na wananchi kwa kuathiri afya zao kutokana na Moshi
unaotoka kiwandani hapo.
Aidha mbele ya umati wa
wafanyabiashara na wananchi katika mkutano huo Mkurugenzi Kayombo
amemuagiza Kaimu Injinia wa Manispaa ya Ubungo kusambaza kifusi cha mawe
kilichomwagwa sokono hapo kwa ajili ya kuzuia mlundikano wa maji.
Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa
serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kukusanya
mapato kwa kiasi kikubwa hivyo ameeleza dhamira yake ya kukusanya mapato
ya Zaidi ya shilingi milioni 150 kwa mwezi katika soko la Ndizi-Mabibo
na tayari mirija na mianya yote ya rushwa amefanikiwa kuiziba kwa kiasi
kikubwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment