Rahim Kwangaya, mkazi wa Mandela, Ikwiriri mkoani Rufiji, ameuawa
kwa kupigwa riasi na watu wasiofahamika, kisha maiti yake kwenda
kutupwa kwenye jalala lililopo kando ya nyumba yake, tukio lililotokea
usiku wa kuamkia juzi.
Katika
tukio hilo, mke wa marehemu, Tatu Mnete, naye alipigwa risasi kwenye
titi la kushoto ambapo alikimbizwa hospitali anakoendelea na matibabu.
Mganga
Mkuu wa Kituo cha Afya cha Ikwiriri, Dkt. Iddy Malinda, alithibitisha
kupokea mwili wa Kwangaya, ukiwa na majeraha mawili ya risasi, tumboni
na kwenye bega ambapo alieleza kwamba baada ya kuufanyia uchunguzi mwili
huo, waligundua pia kwamba ulikuwa na michubuko kichwani, jambo
linaloonesha maiti iliburuzwa baada ya mauaji.
Akaongeza
kwamba walimpokea pia mke wa marehemu aliyekuwa amepigwa risasi kwenye
ziwa, na kwamba alihamishiwa Hospitali ya Mchukwi kwa matibabu zaidi.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum ya Mkuranga, Kibiti na Rufiji, Onesmo Lyanga,
alipotafutwa ili kuthibitisha tukio hilo, alisema hawezi kujibu
chochote kwa sababu hakuwepo ofisini.
Kwa
mujibu wa mashuhuda, wauaji hao walifika nyumbani kwa Kwanganya
anayejishughulisha na biashara maeneo ya Mnadani, ambapo walimuamuru
kufungua mlango na alipofanya hivyo tu, alipigwa risasi na kufa papo
hapo.
SHARE
No comments:
Post a Comment