Aliyekuwa afisa wa
kijasusi wa Urusi alihudhuria mkutano mwaka uliopita na maafisa wakuu wa
rais Donald Trump na mwanawe ,imebainika.
Mwanawe Trump aliahidiwa kupewa habari mbaya dhidi ya mgombea wa chama cha Democrat Hillary Clinton katika mkutano huo , kwa mujibu wa barua pepe zake.
Mwana huyo wa Trump awali alikuwa amekiri kwamba kulikuwa na wakili wa Urusi Natalaia Veselnitskaya aliyehudhuria.
Donald Trump Jr alikuwa amekana kuwepo kwa mkutano uliofanyika tarehe 9 mwezi Juni 2016 , kabla ya kuripotiwa wiki hii.
Lakini kamati ya haki ya bunge la seneti imemtaka mwana huyo mwenye umri wa miaka 39 kutoa ushahidi hadharani.
Majopo kadhaa ya bunge la Congress nchini humo pamoja na majasusi wanachunguza madai kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani mwaka uliopita ili kumsaidia Donald Trump kuibuka mshindi.
SHARE
No comments:
Post a Comment