Serikali ya Uturuki
imewaachisha kazi zaidi ya maafisa 7,000 wa polisi, maafisa wa Serikali
na wasomi waliokuwa na uhusiano na jaribio la mapinduzi la mwaka
uliopita.
Zaidi ya watu 250 waliuawa kabla ya jaribio hilo kuzimwa na wanajeshi walioa waaminifu kwa Serikali.
Hatua hii ni sehemu moja tu ya kuwaondoa watu wasio waaminifu ambapo kufikia sasa zaidi ya watu 200,000 wameachishwa kazi.
Rais Erdogan anawalaumu kwa kuunga mkono wapangaji wa mapinduzi hayo yanayodaiwa kupangwa na kiongozi wa kidini aliye uhamishoni Marekani, Fethullah Gulen.
Bwana Gullen anasema kuwa Rais anasema uongo kuhusiana jaribio na mapinduzi hayo.
SHARE
No comments:
Post a Comment