Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amelitaka
Jeshi la Polisi kumuondoa katika nafasi ya Mkuu wa Polisi Usalama
Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani kutokana kwa kushindwa kusimamia sheria
za usalama barabarani mkoani humo.
Masauni
alitoa agizo hilo katika Kituo cha Mabasi cha mjini Kibaha Maili Moja
baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo jana, kwa ajili ya
kufuatilia maelekezo yake aliyoyatoa alipofanya ziara kama hiyo mwaka
jana.
“RTO
ameshindwa kuendana na kasi ya awamu ya tano, nataka aondolewe katika
nafasi hiyo na achukuliwe hatua ya kinidhamu, hatutaki uzembe, hatutaki
kucheza na maisha ya watanzania,” alisema Masauni.
“Mwaka
jana nilipofanya ziara kituoni hapa nilitoa maelekezo nilipokuta kuna
mapungufu katika ukaguzi wa magari, tukakubaliana atayafanyia kazi
haraka iwezekanavyo, lakini hakuna mabadiliko yoyote, magari
hayakaguliwi, huku ni kuhatarisha usalama wa abiria.”
Aidha
Masauni mara baada ya ukaguzi wa kituo hicho, aliendelea na ziara yake
mkoani Pwani ambapo alifanya ukaguzi wa aina hiyo mjini Chalinze na
baadaye Msata na kuimalizia ziara yake Bagamoyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment