Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa umma na viongozi wa dini wa
mkoa wa Songwe kwenye ukumbi wa Chuo cha Uuguzi cha Kanisa Katoliki cha
Mwambani wilayani Songwe, Julai 20, 2017. Kushoto ni Mkewe Mary na Katikati ni
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku GalaWa.(PICHA
NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
NA OFISI YA WAZIRI
MKUU, SONGWE
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amempa miezi miwili kuanzia leo Mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya ya Songwe, Bw. Elias Nawera abadili mwenendo wake
kiutendaji na ashirikiane vizuri na Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Samwel
Jeremiah.
Amesema Serikali ya awamu ya Tano inawataka watumishi wote kufanya kazi
kwa ushirikiano na kuheshimiana na atakayeshindwa kufanya hivyo hatavumiliwa.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Julai 20, 2017) wakati
akizungumza na watumishi wa wilaya ya Songwe akiwa katika ziara yake ya kikazi
mkoani Songwe.
Amesema watumishi wote wanatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili
malengo ya Serikali ya kuwahudumia wananchi yaweze kufikiwa. Pia waheshimiane
sehemu za kazi na kila mtu azingatie mipaka ya madaraka yake.
"Mkurugenzi hapa hamsikilizi Mkuu wa wilaya anaondoka kituo cha kazi
bila ya kuaga na amewagawa wakuu wa Idara. Namtaka afanye mabadiliko ya
utendaji wake ndani ya miezi miwili na Mkuu wa Mkoa fuatilia jambo hili."
Pia amewaagiza Wakuu wa Wilaya wote wasimamie utendaji wa wakurugenzi wa
Halmashauri kwenye maeneo yao ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa
ipasavyo.”Serikali hii si ya mchezo. Serikali hii inahitaji watumishi waadilifu
wa kuwatumikia Watanzania.”
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Bibi Chiku Galawa amesema
wamejipanga kuhakikisha changamoto zote zinazoukabili mkoa zinaboreshwa pamoja
na kufikia malengo ifikapo 2020.
Ametaja malengo hayo kuwa ni kuhakikisha mkoa huo unakuwa kinara katika
ukusanyaji wa mapato, kila mwananchi awe na bima ya afya pamoja na kuwa na
hospitali katika kila wilaya.
Kuhusu mpango wa Serikali wa kuwa na uchumi wa viwanda amesema tayari
wameshaanzisha viwanda vya maziwa, kukamua alizeti ikiwa ni kuunga mkono mpango
huo.
Mke
wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisalimia wakati Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa (kulia) alipozungumza na watumishi wa umma na viongozi wa dini
kwenye ukumbi wa Chuo cha Uuguzi cha Kanisa Katoliki cha Mwambani
wilayani Songwe, Julai 20, 20117. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku
Galawa
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa baada
ya kuwasili Mkwajuni wilayani Songwe kuanza ziara ya mkoa wa Songwe Julai 20,
2017. Kulia ni mkewe Mary.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Songwe,
Elias Nawela baada ya kuwasili Mkwajuni wilayani Songwe kuanza ziara ya
mkoa wa Songwe Julai 20, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku
Galawa.
Baadhi
ya watumishi wa umma na viongozi wa dini wa mkoa wa Songwe wakimsikiliza Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye ukumbi wa Chuo cha
Uuguzi cha Kanisa Katoliki cha Mwambani wilayani Songwe, Julai 20, 2017.

SHARE
No comments:
Post a Comment