Jenerali Abdul Rashid Dostun aijiunga na serikali ya muungano ya Afghanistan
Makamu wa rais wa
Afghanistan Abdul Rashid Dostun alijaribu kurudi nchini humo baada ya
kusafiri kuelekea Uturuki lakini ndege yake ikakatazwa kutua nchini humo
kulingana na maofisa.
Jenerali Dostun aliondoka nchini Uturuki mnamo mwezi Mei huku kukiwa na madai kwamba aliwaagiza watu wake kumteka, kumpiga na hata kumbaka mpinzani wake wa kisiasa.
Amekana kufanya makosa yoyote.
Msemaji wake anasema kuwa alielekea Uturuki kwa ukaguzi wa afya yake.
Atta Mohammad Noor , ambaye ni gavana wa kaskazini mwa mkoa wa Balkh ,alikuwa akisubiri katika uwanja wa ndege wa Mazar-e Sharrif kumpokea Jenerali Dostun siku ya Jumatatu usiku, kulingana na chombo cha habari cha Pajhwok.
Zaidi ya watu 1000 waliandamana na gavana huyo kumpokea mpiganaji huyo wa zamani katika mpaka huo ambao uko karibu na mkoa wa nyumbani wa Jowzjan.
Mashahidi wanasema kuwa baadhi ya wafuasi wa Dostun walikuwa na mabango yaliosema karibu nyumbani kiongozi wetu, kulingana na chombo cha habari cha Reuters.
SHARE









No comments:
Post a Comment