TRA

TRA

Wednesday, July 5, 2017

NI AIBU. NUSU YA WAHAMIAJI NI WATOTO KUTOKA AFRIKA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Zaidi ya watoto milioni 7 kutoka nchi za Afrika Magharibi pamoja na Afrika ya Kati wanakimbia vurugu, umaskini na mabadiliko ya tabianchi, idadi ambayo ni zaidi ya nusu ya wahamiaji wote wanaotoka katika kanda hiyo, kulingana na taarifa za leo za Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto ( UNICEF). 

Wengi kati ya watoto hao wanatafuta hifadhi katika nchi nyingine barani Afrika, na ni mmoja tu kati ya watoto watano anayejaribu kwenda barani Ulaya, kulingana na ripoti ya shirika la UNICEF. 

Watu wapatao nusu milioni wamevuka Bahari ya Mediterenia kupitia nchini Libya hadi Italia katika kipindi cha miaka minne iliyopita, wengi wakitokea nchi za Kiafrika zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara.

CHANZO: DW

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger