BAADA
ya Jumamosi iliyopita Mbunge wa Mikumi kwa tiketi ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule ‘Profesa Jay’ kufunga
ndoa na mchumba’ke wa kitambo, Grace Mgonjo katika Kanisa la Mtakatifu
Joseph lililopo Posta jijini Dar na sherehe kufanyika ndani ya Ukumbi wa
Mlimani City, ameibuka na kufunguka suala la Miss Tanzania 2006/07,
Wema Sepetu kuikacha harusi yake.
Taarifa
za awali kutoka kwa chanzo makini zilieleza kuwa, Profesa Jay na Wema
ambaye alihamia Chadema miezi kadhaa iliyopita wana bifu kali japokuwa
haijulikani chanzo ni nini, ndiyo maana mwanadada huyo hakuhudhuria
kwenye harusi hiyo.
“Unajua
Wema na Jay hawana uhusiano mzuri tangu ahamie kwenye chama hicho yaani
wana bifu ndiyo sababu hata Wema hakuhudhuria kwenye sherehe ya harusi
ya Jay maana wangekuwa sawa ungeona mbwembwe zake ukumbini lakini
hakutokea,” kilidai
chanzo hicho.
Baada
ya kuzinyaka habari hizo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Profesa Jay kwa
njia ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp akiwa honeymoon ambapo mahojiano
yalikuwa hivi;
Risasi Jumamosi: Hongera kwa kuoa na kuachana na ubachela Jay. Profesa
Jay: Asante sana, karibu.
Risasi Jumamosi: Kuna habari kuwa wewe na Wema mna bifu ndiyo maana hakuhudhuria hata kwenye harusi yako, hili likoje?
Profesa Jay: Jamani watu hawaishiwi maneno! Wema ni kamanda wangu tena tunahesh
imiana kwelikweli nisizuliwe bifu zisizokuwa na kichwa wala miguu.
Risasi Jumamosi: Kwa nini sasa hakuwepo au hukumwalika?
Profesa
Jay: Mbona kuna watu wengi tu hawakuhudhuria kwa nini Wema? Mwacheni
dada yangu apumzike, acha hizo stori. Profesa Jay kwa upande mwingine
alieleza kuwa kesho Jumapili anatarajia kufanya sherehe kubwa kuliko ya
mwanzo huko jimboni kwake Mikumi ambayo kila mwananchi atahudhuria kwani
hakutakuwa na kadi na itafanyika uwanjani ikiwa ni shukrani kwao kwa
kumchagua kuwatumikia
SHARE
No comments:
Post a Comment