Rais
Dkt John Pombe Magufuli akipewa akisikiliza maelezo mafupi mara baada
kufungua mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Tabora.
Rais Dkt Magufuli ameagiza Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano
kujenga jengo la abiria 500 badala ya jengo lililopo la abiria 50.Pia
ameagiza urefu wa uwanja uongezwe hadi kufikia kilometa 2.5 badala ya
kilometa 1.9 zilizopangwa ili ndege kubwa na ndogo ziweze kuutumia
uwanja huo.
Rais
Dkt John Pombe Magufuli ameweka jiwe la Msingi la mradi wa maji kutoka
Ziwa Victoria kwenda miji ya Tabora, Nzega na Igunga. Mradi huo
utagharimu Shilingi Bilioni 600 na unatekelezwa kwa fedha za mkopo nafuu
kutoka India. Una uwezo wa kuzalisha lita Milioni 80 kwa ajili ya Mji
wa Tabora.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo mafupi ya mradi hu wa
ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Tabora,kutoka kwa Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Prof Makame Mbarawa mapema leo mkoani
humo
Rais
Dkt John Pombe Magufuli mapema leo amefungua mradi wa ukarabati na
upanuzi wa uwanja wa ndege wa Tabora,Wakati wa uzinduzi wa mradi
huo,Rais Dkt Magufuli ameagiza Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano
kujenga jengo la abiria 500 badala ya jengo lililopo la abiria 50.Pia
ameagiza urefu wa uwanja uongezwe hadi kufikia kilometa 2.5 badala ya
kilometa 1.9 zilizopangwa ili ndege kubwa na ndogo ziweze kuutumia
uwanja huo.
SHARE
No comments:
Post a Comment