Rais
John Magufuli amesema Serikali haitatoa chakula kwa mkoa utakaokumbwa
na baa la njaa na badala yake viongozi wa mkoa huo watawajibishwa.
Ameyasema
hayo leo Jumanne, Julai 25 wakati wa ziara yake ya uzinduzi wa barabara
na kuongeza kuwa kiongozi ambaye hatahamasisha watu wake kulima hafai
kuwa kiongozi.
“Wilaya
ikiwa na njaa nitajua wewe mkuu wa mkoa hufai, mkuu wa wilaya hufai.
Mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya atakayeshindwa kuwahamasisha watu wake
wafanye kazi, hafai kuwa kiongozi,” amesema.
Amewataka wakuu wa mikoa kuwaondoa katika nafasi zao makatibu tarafa ambao hawahamasishi kilimo.
“Ikiwezekana
na wewe mkuu wa wilaya au mkoa, kama unakaa kijijini au ni katibu kata
onyesha mfano wako wa kazi. Ukiwa diwani, hivyo hivyo, ukiwa mbunge
hivyo hivyo. Ndiyo maana ninatimiza wajibu wangu wa kuhamasisha watu,
chapa kazi, hapa kazi tu.” Amesema.
SHARE
No comments:
Post a Comment