TRA

TRA

Tuesday, July 18, 2017

Seneta aliyemnyonyesha mtoto bungeni ajiuzulu Australia

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Waters akimnyonyesha binti yake Alia Joy mwezi mei
 
Seneta aliyeandikisha historia nchini Australia kwa kumnyonyesha mtoto bungeni amejiuzulu baada ya kugundua kwamba ana uraia wa nchi mbili.

Larissa Waters, kutoka kwa chama cha Greens, alizaliwa nchini Canada. Chini ya katiba ya Australia, mtu haruhusiwi kuwania wadhifa wowote katika serikali ya taifa iwapo ana uraia wa nchi mbili na zaidi.

Ijumaa, seneta mwingine wa chama cha Greens, Scott Ludlam, alijiuzulu pia kwa sababu ya kuwa na uraia wa nchi mbili.
Wanasiasa wote wawili walikuwa manaibu viongozi wa chama hicho.
Mwezi mei, Bi Waters alipata umaarufu kimataifa baada ya kuwa mwanasiasa wa kwanza kumnyonyesha mtoto katika bunge la Australia.
'Sikujua'
Bi Waters anasema aligundua hali yake ya uraia baada ya kuibuliwa kwa kisa cha Bw Ludlam, ambaye aligundua majuzi kwamba yeye ana uraia pia wa New Zealand.

Huku akijizatiti kuzuia machozi katika kikao cha wanahabari Jumanne, Bi Waters alisema lilikuwa kosa lisilo la kukusudia. 

"Nilisikitika sana kugundua kwamba kwa sababu ya sheria za miaka 70 nchini Canada, nimekuwa na uraia wa nchi mbili tangu kuzaliwa kwangu, na kwamba sheria nchini Canada ilibadilishwa wiki moja baada ya kuzaliwa kwangu. Sheria mpya ilinitaka kuukana uraia wangu wa Canada," alisema.

Seneta huyo ambaye sasa ana miaka 40, alikuwa na umri wa miezi 11 alipoondoka Canada akiwa na wazazi wake ambao ni raia wa Australia. "Yote haya yalitokea kabla hata niweze kutamka neno la kwanza," alisema.

Hata hivyo, Waters, ambaye alichaguliwa mara ya kwanza 2011, amesema anakubali lawama.

Haijabainika iwapo yeye pamoja na Bi Ludlam watalipa pesa ambazo wamepokea kama mshahara na marupurupu katika kipindi ambacho wamehudumu.

Kwa mujibu wa katiba ya Australia, mwanasiasa ni lazima aukane uraia wake wa nchi ya nje kabla ya kuwania wadhifa wa kisiasa.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger