Kampuni ya simu ya maisha ya kidigitali inayoongoza
Tanzania, Tigo, Pamoja na wabia wengine, wameshirikiana katika
kufanikisha upatikanaji wa mtandao wa broadband kwa watu takribani
70,000 katika maeneo yaliyochaguliwa katika maeneo ya vijijini ya
Tanzania.
Ushirikiano na waendeshaji wengine wa mitandao ya simu (MNOs) (Mobile network Operators), serikali ya Tanzania na Chama cha kutetea maslahi ya waendeshaji wa mitandao ya simu duniani GSMA (Global System Mobile Association), uliundwa
kutatua changamoto za upatikanaji wa mtandao katika maeneo ya vijijini
kwa kuanzisha maeneo ya majaribio kama sehemu inayokusudiwa ya mradi wa
upatikanaji wa mawasiliano.
Katika
ujumbe wake katika kongamano linaloendelea la GSMA la 360 – Afrika
lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es
salaam leo, Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Bwana
Simon Karikari, alisema kwamba ni kwa kutumia ushirikiano wa sekta ya
umma na sekta binafsi ndipo ambapo tunaweza kukabiliana na changamoto za
kidigitali, hivyo kukuza mageuzi ya kidigitali ya Afrika.
“Kutoa
uunganishaji wa simu wa Broadband kwa jamii za vijijini ni moja kati ya
changamoto kubwa ambazo waendeshaji wanakabiliana nazo hapa Tanzania
leo. Hii ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo: Upatikanaji wa Umeme,
Mgawanyiko wa watu kijiografia, na uwezo wa kumudu gharama – hata
ambapo huduma za data ni moja kati ya huduma za bei nafuu zaidi katika
eneo hilo”, alisema Karikari.
Akielezea
kuhusu ushirikiano, Karikari amesema kwamba wameingia katika
makubaliano ya pande tatu ya roaming ambayo maeneo ya majaribio
yatawezesha upatikanaji wa mtandao wa broadband kwa wateja wa mitandao
yote kutoka katika mnara mmoja, jambo ambalo litawasaidia watumiaji
kutumia mitandao ya kila mmoja wao katika eneo lililochaguliwa.
Mkurugenzi
alipongeza ushirikiano wa sekta zaidi ya moja akieleza kwamba
ushirikiano huo umewezesha kufanikisha mradi wa roaming wa njia tatu
Afrika.
“Kudokeza
baadhi tu ya matokeo yetu”, Karikari aliongeza kwamba, “Tayari kulikuwa
na watumiaji 17,000 wa simu kila siku baada ya uzunduzi. Leo zaidi ya
wakaazi elfu 40 wa maeneo ya vijijini wanapata huduma ya 3G kwa mara ya
kwanza, idadi inakadiriwa kuongezeka kufikia elfu 70 kufikia mwishoni
mwa mwezi Juni 2017).
Akishukuru
serikali ya uungaji mkono wake katika kutekeleza mradi huu, Hata hivyo
Karikari alisema kwamba, aina fulani ya ruzuku, motisha na makubaliano
kama vile kodi katika miundombinu kutoka serikalini, inakaribishwa
kusaidia MNOs kupungaza baadhi ya gharama zinazotokana na uanzishaji wa
maeneo ambayo hayaja lipwa na mapato yanyotokana na mradi.
“Tunaamini
kwamba mradi huu, pamoja na upekee wake, utaweka uwezekano kwa bara
zima la Afrika. Tutaendelea kushirikiana na Serikali, TCRA (Mamlaka ya
Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania), UCSAF (Mfuko wa upatikanaji
wa huduma ya mawasiliano Tanzania), na taasisi zingine kutafuta
ufumbuzi wa changamoto tulizo zigundua na kuangalia namna tutakavyotumia
tuliyojifunza kutoka katika mradi huu kuboresha huduma zetu na hatimaye
kuleta uunganisho wa simu Tanzania”. Alihitimisha Karikari
Tigo kuungana na wabia wengine kuongeza kasi katika upatikanaji wa Mtandao wa simu kwa wananchi 70,000 katika maeneo ya vijijini Tanzania

SHARE
No comments:
Post a Comment