Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb)
(wa tano kulia) akiwa katika eneo la Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda kipya
cha viatu cha Karanga Leather Industries Ltd Karanga Moshi, kinatarajiwa
kujengwa kwa ubia kati ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF na Jeshi la
Magereza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb)
(katikati) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika
Kiwanda cha Viatu Karanga Moshi. Kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe.Dkt. Philipo Mpango (Mb) na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
Mhe. Anna Mghwira. Kiwanda cha viatu Karanga kinatarajiwa kupatiwa
teknolojia mpya kutoka PPF itakayokiwezesha kuongeza uzalishaji kutoka
Jozi 150 za sasa za viatu hadi jozi 400 kwa siku.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb)
wa tatu kulia, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philipo Mpango (Mb)
(wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi
Hamad Masaun (Mb) kwa pamoja wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa
mafundi wa utengenezaji wa viatu kiwandani hapo leo tarehe 14 Julai,
2017 Karanga Moshi.
Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe.Dkt. Philipo Mpango (Mb) akiangalia moja viatu vinavyozalishwa na
Kiwanda cha Viatu Karanga Moshi alipotembelea kiwanda hicho pamoja na
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu
wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) pamoja na Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masaun (Mb) na Katibu Mkuu Wizara ya
Viwanda na Uwekezaji Prof, Adolf Mkenda.leo tarehe 14 Julai, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb)
akichukuliwa vipimo kwa ajili ya kutengenezewa viatu alipotembelea
Kiwanda cha Viatu Karanga Moshi leo tarehe 14 Julai, 2017.
Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe.Dkt. Philipo Mpango (Mb) na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Mhandisi Hamad Masaun wakichukuliwa vipimo vya miguu kwa ajili ya
kutengenezewa viatu walipotembelea Kiwanda cha Viatu Karanga Moshi.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philipo Mpango (Mb) (wa kwanza kushoto) meza kuu akifafanua jambo
katika kikao cha ndani kilichofanyika kiwandani Karanga Moshi mara baada
yeye na Waziri Jenista Mhagama na Naibu wa Waziri Hamad Masaun kufanya
ziara katika eneo la Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda Kipya na Kiwanda cha
sasa cha viatu cha Karanga Moshi leo tarehe 14 Julai, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb)
akitoa hotuba fupi kwa wageni waalikwa, baadhi ya viongozi wa Jeshi la
Magereza, PPF na Wajumbe wa Bodi ya Karanga Leather Industries Ltd
(hawapo pichani) ikiwa ni majumuisho ya ziara yake ya Kutembelea Miradi
ya Uwekezaji wa Ubia kati ya Jeshi la Magereza na Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii wa PPF, leo katika Ukumbi wa Gereza Karanga Moshi. (Wa pili kulia)
ni Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt, Juma Malewa na (wa pili kushoto)
ni Mkurugenzi Mkuu Wa PPF Ndg.William Erio.
Baadhi ya Maafisa wa Magereza na
wafanyakazi wa PPF wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mh.
Jenista Mhagama (Mb) (hayupo pichani) katika Ukumbi wa Magereza Karanga
Moshi.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia hotuba ya Mgani
Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu
wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) (hayupo pichani) (wa Kwanza
kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa
Mwandamizi wa Magereza (SACP) Hamis Nkhubasi na (wa kwanza kushoto) ni
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza
(SACP) Julius Ng’udi
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya
Karanga Leather Industries Ltd wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi baada
ya kufanya ziara ya kutembelea miradi ya uwekezaji kati Jeshi la
Magereza na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF. (wa kwanza kulia) ni
Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga.
SHARE
No comments:
Post a Comment