Eneo la mto Nyakasangwe lililopo
kaika kata ya Bunju linavyoonekana kuharibika vibaya kutokana na
uchimbaji wa mchanga , na kupelekea makazi ya wananchi kuwa hatarini.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akizungumza na vyombo vya
habari baada ya kukamilika kwa zoezi la kukagua mto Nyakasangwe, uliopo
katika kata ya Bunju ulioharibiwa vibaya na uchimbaji wa mchanga.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akimsikiliza Mwandishi wa
Habari wa kituo cha Radio cha Efm kinachopatikana katika masafa ya 93.7
katika jiji la Dar es Saalam alipokuwa akimuuliza maswali kuhusu
uchafuuzi wa mazingira utokanao na uchimbaji wa mchanga katika eneo la
Boko.
……………………………………………………………….
NA; EVELYN MKOKOI
NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina ,amesitisha uchimbaji na
uchotaji wa mchanga kiholela katika maeneo yasiyo rasmi.
Pia ametoa siku 30 kwa
Halmashauri za Manispaa za Jiji la Dar es Salaam kubaini na kutenga
maeneo ya uchimbaji ya mchanga ambayo yapo ndani ya manispaa zao
yatakayo ruhusiwa kwa zoezi hilo kisheria.
Akitoa agizo hilo Dar es Salaam jana wakati wa ziara ya kutembelea Mto Nyakasangwe uliopo maeneo ya Boko
Kata ya Bunju alisema kama kuna maeneo ambayo wananchi wanaweza kufika
Kwa urahisi, manispaa zinapaswa kuyatembelea maeneo hayo na kuyabaini
kama kunauwezekano wakuchimba mchanga.
Alisema ndani ya mwezi mmoja
manispaa hizo zinatakiwa kuandaa utaratibu mfupi wa kutenga maeneo hayo
ikiwemo utoaji wa vibali kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Halmashauri
pamoja na Nemc.
“Halmashauri zote zilizo na eneo
ambalo linaweza kuruhusiwa kuchota mchanga hakikisheni mnatembelea
maeneo hayo na kufata taratibu zote za utoaji wa vibali ambapo maeneo
mengine yawe ya uchotaji wa mchanga,”alisisitiza Mpina
Alisema watafanya Operasheni ya
usiku na mchana kuhakikisha watu watakaoendelea kuchimba mchanga na
kuchota mchanga sehemu ambazo haziruhusiwi watachukuliwa hatua ikiwa ni
pamoja na kutozwa faini zilizopo kisheria na kufikishwa mahakamani.
Kwa upande wake diwani wa kata ya
Bunju Bw. Kateni Nassor Msangi alimshukuru Mpina kwa kufanya ziara
katika eneo hilo na kuiomba serikali kufanya utaratibu wa kujengea mawe
katika kuta za kingo yam to huo ambao umeharibika vibaya, ili kuweza
kunusuru mazingira ya mto huo kuharibika pamoja na kunusuru makazi yao
SHARE








No comments:
Post a Comment