Na Karama Kenyunko.
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imewasomea upya mashtaka, washtakiwa Harbinder
Singh Sethi na James Burchard Rugema rila kwa kuwaongezea mashtaka na
kufanya idadi yao kufikia 12.
Mapema mwezi uliopita, washtakiwa hao walipandishwa kizimbani hapo baada ya kusomewa mashtaka sita kabla ya leo kuwa 12.
Katika
mashtaka hayo ambayo ni ya uhujumu uchumi yapo pia matano ya
utakatishaji wa fedha na kuisababishia Serikali hasara ya USD 22,
198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.
Mashtaka
hayo ni, kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu , kughushi,
kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu
kuisababishia Serikali Hasara na kutakatisha fedha.
Washtakiwa wamesomewa mshtaka yao mapya na wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.
Katika
shtaka la kwanza inadaiwa, Rugemarila Mkurugenzi wa VIP na mmiliki
mwenza wa zamani wa IPTL na Sethi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa PAP,
kati ya oktoba 18 ,2011 na Machi 19 , 2014 jiji Dar es Salaam walikula
njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha
kwa njia ya udanganyifu.
Imedaiwa
kuwa, Oktoba 18,2011na Machi 19,2014 washtakiwa hao wakishirikiana na
watumishi wa umma walitekeleza mtandao huo wa uhalifu kwa lengo la
kujipatia faida.
Aidha
katika shtaka la tatu linalomkabili Sethi peke yake imedaiwa, Oktoba
10,2011 katika mtaa wa Ohio Ilala, akiwa na nia ya ulaghai alighushi
fomu namba 14 a ya usajili wa makampuni na kuonyesha yeye ni mtanzania
anayeishi Kitalu namba 887 Mtaa wa Mrikau Masaki wakati akijua ni uongo.
Seth
pia anadaiwa kutoa nyaraka ya kughushi ambayo ni fomu namba 14a ya
usajili wa kampuni kwa ofisa msajiri wa kampuni,Seka Kasera kwa njia ya
kuonesha kwamba yeye ni mtanzania na Mkazi wa Mtaa wa Mrikau.
Imeendelea
kudaiwa kuwa, Novemba 28/29, 2011 na Januari 23,2014 katika Makao Makuu
Benki ya Stanbic Kinondoni na Benki ya Mkombozi tawi St Joseph kwa
ulaghai washtakiwa hao walijipatia kutoka Benki Kuu ya (BOT),
walijipatia USD 22,198,544.60 na Tsh 309, 461,300,158.27.
Aidha wanadaiwa kuisababisha hasara, serikali ya kiasi hicho cha fedha.
Katika
shtaka la saba, inadaiwa kati Novemba 29,2013 na January 23, 2014
maeneo tofauti Dar es Salaam kwa pamoja walitakatisha fedha kwa kuchukua
fedha kutoka BOT USD 22,198,544.60 na Tsh 309,461,300.27 wakati wakijua
fedha hizo zao la kujihusisha na genge la uhalifu.
Sethi
peke yake anadaiwa pia kuwa Novemba 29,2013 katika tawi la kati la
Benki ya Stanbic Tanzania wilaya ya Kinondoni, alitakatisha fedha kwa
kuchukua BOT USD 22,198,544.60 wakati akijua fedha hizo zimetokana na
zao la kujihusisha na genge la uhalifu.
Aidha
Sethi anadaiwa kutakatisha shilingi 309,461,300,158.27 kutoka BOT
wakati akijua fedha hizo zimetokana na zao la kujihusisha na genge la
uhalifu.
Katika
shtaka la kumi, inadaiwa Januari 23, 2014 katika Benki ya Mkombozi tawi
la St Joseph Cathedral, Rugemarila alitakatisha, Sh 73,573, 500,000
kutoka kwa Seth wakati akijua fedha hizo zimetokana na zao la
kujihusisha na genge la uhalifu.
Kwa
upande wa shtaka la 11, Kimaro alidai kuwa Januari 23,2014 katika benki
ya Mkombozi tawi la St Joseph Cathedral, Rugemarila alitakatisha fedha
USD 22,000,000 kutoka kwa Seth wakati akijua fedha hizo ni zao la
uhalifu.
Shtaka
la 12, Seth anadaiwa kuwa Januari 28,2014 katika tawi la kati la Benki
ya Stanbic wilaya ya Kinondoni alihamisha Rand (zar 1,305,800 kwenda
kwenye akaunti namba 022655123 katika Standard bank Land Rover Sandton
Johannesburg wakati akijua katika kipindi anahamisha fedha hizo
zimetokana na zao la kujihusha na genge la uhalifu.
Washtakiwa
hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote kwa sababu mahakama ya Kisutu haina
mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na washtakiwa wamerudishwa rumande kwa
kuwa mashtaka ya utakatishaji wa fedha hayana dhamana.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo itatajwa tena Julai 14,201.
Mtuhumiwa James Burchard Rugemarila akirejeshwa rumande
Mtuhumiwa Harbinder Singh Sethi wakirejeshwa rumande
SHARE
No comments:
Post a Comment