Abdulazizi Chende, ‘Dogo Janja’ amefunguka kuwa bila yeye mshindani wake mkubwa katika muziki huo, Erick Msodoki “Young Killer’ hawezi kufika popote maana atakosa kiki na zaidi atakufa njaa.
Akichonga na Uwazi Showbiz, Dogo Janja alisema kuwa amemfuatilia Young Killer katika
kazi zake na kugundua kuwa kabla ya kutoa ngoma mpya ni lazima atafute
kiki kupitia yeye jambo ambalo limemfanya kumdharau na kumuona kuwa ni
msanii ambaye anapenya kwa kutumia mgongo wake.
“Bila
mimi yule bwana mdogo atakufa njaa, nimejaribu kumchunguza kila
anapotaka kutoa ngoma mpya ni lazima atafute kiki kupitia mimi, iwe
kwenye media ama kwenye mitandao ya kijamii, kwa hiyo kwa upande wangu
naona jamaa hawezi kusimama mwenyewe,” alisema Dogo Janja
SHARE
No comments:
Post a Comment