"Mimi natoa nyimbo zangu kulingana na jinsi ambavyo nimepanga ratiba
yangu na uongozi wangu. Sijashindwa kuachia wimbo eti kwa sababu Aslay
katoa ngoma mpya ila matatizo niliyopata ya kupelekwa polisi ndiyo
yaliyonifanya nisogeze vitu mbele," Beka alifunguka mbele ya kamera za
eNewz
Beka aliongeza kuwa "Aslay siyo msanii mkubwa kusema kwamba mimi
nimuogope au nimfikirie. Hapa nchini msanii mkubwa ni Alikiba na ndo
kama kioo najitazama lakini siyo Aslay. Mimi natazama wasanii wakubwa
nje ya nchi lakini siyo ndugu yangu".
Mwanamuziki
anayefanya vizuri na ngoma yake ya 'Nibebe', Beka Flavour amefunguka na
kusema Aslay siyo msanii mkubwa wa kumuangalia wakati anafanya kazi
zake na badala yake Alikiba ndiye kioo chake kwa Tanzania.
Beka amelazimika kusema hayo baada ya kuwepo minong'ono kuwa huenda
anamuogopa msanii huyo ambaye zamani walikuwa wakifanya kazi pamoja kama
kundi la 'Yamoto Band' kabla ya kila msanii kuanza kusimama mwenyewe.
Pamoja na hayo Beka amedai hataweza kumvumilia tena msanii huyo ambaye
amefululiza kutoa nyimbo nyingi hivi karibuni endapo ataachia tena kazi
mpya.
"Nimepanga kuachia wimbo mpya wiki mbili zijazo lakini kama Aslay
akiachia tena kazi mpya sitaweza kumvumilia na mimi nitaachia mashine
ili zipambane mbele kwa mbele maana mimi nimeshapanga ratiba zangu na
siwezi kuzivunja," aliongeza.
SHARE
No comments:
Post a Comment